Ugeni kutoka Ataba tukufu wamaliza ziara yao kaskazini ya Pakistani na wakazi waomba kuendelea kwa ziara kama hii na matoleo ya kielimu yaandikwe zaidi kwa lugha ya kiurdu..

Maoni katika picha
Ugeni wa Ataba tukufu za (Alawiyya, Husseiniyya na Abbasiyya) ulio enda kaskazini ya Pakistani hadi katika milima ya Hamlaya, ambako kuna makumi ya vijiji vinavyo zunguka milima hiyo vikiwa na idadi kubwa ya wapenzi wa Ahlulbait (a.s), upepo wa barafu uliopiga ulisababisha kuahirishwa baadhi ya mambo yaliyo pangwa katika ziara hiyo, iliyo dumu kwa siku sita.

Wakazi wa miji hiyo wameubebesha ujumbe wa wageni maombi mengi ambayo wamewataka wayafikishe katika Ataba tukufu za Iraq, na wameomba kuendelea kwa ziara za aina hii, kwani miji yao ni migumu kufikika, pia wameomba kutolewa machapisho ya Ataba kwa lugha ya urdu na kuyafikisha katika miji yao, wamesisitiza kua wana haja nayo zaidi na yatachangia sana katika kuinua kiwango chao cha elimu ya dini katika jamii zao na kuwalinda wasidumbukie katika magenge yanayo potosha dini ya kiislamu tukufu.

Siku ya mwisho ya ziara ilishuhudia ongezeko kubwa la watu, ratiba ya siku ya mwisho ilianzia katika shule ya wanawake, ambapo wanafunzi walifanya hafla ya kupokea wageni, mjumbe wa ugeni wa Atabatu Husseiniyya tukufu dokta Imani Mussawiy alisisitiza katika ujumbe wake aliotoa kwa wanafunzi wa shule hiyo umuhimu wa kushikamana na mafundisho ya Ahlulbait (a.s) na kuiga tabia za bibi mtakasifu Fatuma Zaharaa (a.s), na kujilinda na magenge yanayo jitokeza katika jamii hivi sasa na kuwarubuni wanawake wakiislamu, wanajua wakimuharibu mwanamke watakua wameharibu jamii nzima kwa sababu mwanamke ndio msingi mkuu wa malezi ya familia.

Kituo cha pili kilikua katika majengo ya Ahlulbait (a.s) makazi ya mayatima, linalo simamiwa na muwakilishi wa Marjaa dini mkuu katika nchi ya Pakistan muheshimiwa Shekh Muhsin Ali Najafiy, na ikapandishwa pendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika majengo hayo, rais wa ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh Aadil Wakil aliongea na wakazi wa hapo na kuwasisitiza kuhusu umuhimu wa subira katika mitihani, na kuifanya mitihani kua sababu ya mafanikio na maisha bora, na mafundisho ya Ahlulbait (a.s) kua ndio njia yetu katika maisha, na tuzingatie na kushikamana na maelekezo ya Marjiiyya dini wakuu kwani wao ndio wasimamizi wakuu katika jamii zetu, tukio la mwisho kuhudhuriwa na ugeni huu kilikua ni kikao (majlisi) ya mashairi ya kiurdu iliyo fanyika katika mji wa Sakardu katika mnasaba wa kuzaliwa kwa imamu Zainul-abidina (a.s).

Tunapenda kusema kua ilipo fika jioni ya siku ya Juma Pili (4 Rajabu 1438 h) sawa na (2 April 2017 m) ratiba ya wiki ya kitamaduni awamu ya nne (Nasimu Karbala) ilihitimishwa, program hii iliendeshwa na Atabatu Husseiniyya tukufu kwa kushirikiana na Jaamiatul Kauthara ya Pakistan, na kwa kushiriki Ataba tukufu za (Alawiyya, Askariyya na Abbasiyya) kuanzia tarehe (29 Machi) hadi (2 April), ugeni ulienda kaskazini ya Pakistan hadi katika milima ya Hamlaya iliyopo kaskazini ya mbali ya Pakistan, inayo zungukwa na makumi ya vijiji vyenye wapenzi wengi wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: