Mapokezi ya halaiki kwa wageni wa Ataba tukufu za Iraq katika mji wa Kalkata India..

Maoni katika picha
Umepewa hadhi kubwa ugeni wa Ataba tukufu za Iraq (Alawiyya, Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya) utakao shiriki katika kongamano la Amirulmu-uminina la kitamaduni awamu ya tano, litakalo fanyika katika mji wa Kalkata nchini India na ratiba rasmi ya kongamano hilo itaanza kesho siku ya Juma Tano (14 Rajabu 1438 h) sawa na (12 April 2017 m), wamepata mapokezi makubwa kutoka kwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s) katika mji litakapo fanyika kongamano hili, inapo patikana husseiniyya ya Utukufu wa mwanamke (Fadhlu Nisaai), ambalo linasimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mwaka wa tano mfululizo, kama sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa imamul Muttaqina, Maula Muwahidina, Qaaidul Ghurri Muhajjilina, Waswii Rasulu Rabbil Aalamina, Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s).

Pamoja na kufika usiku mwingi, lakini wenyeji wao waliendelea kuwasubiri hadi wawapokee wageni wao mabalozi wa Ataba za maimamu wao (a.s).

Kama ilivyo ada ya wahindi waliwapokea wageni wao kwa nyimbo na mapambio zikiambatana na swalatu ala nnabi na Ahlubait wake (a.s) pamoja na kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu aliye uteua mji wao miongoni mwa miji mingi iliyo toa maombi ya kua wenyeji wa kongamano hili tukufu, wao wamekubaliwa kua wenyeji wa kongamano hili tukufu ambalo ni sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s).

Kumbuka kua kongamano litafanyika katika husseiniyya ya Utukufu wa mwanamke (Fadhlu Nisaai) katika mji wa Kalkata nchini India kuanzia tarehe: 14 – 19 ya mwezi wa Rajabu 1438h, chini ya kauli mbiu isemayo: (Amirulmu-uminina (a.s) ni hoja kwa waja na muongoaji katika wema) litakua na ratiba nyingi, kamati ya maandalizi ya kongamano hili ilianza maandalizi muda mrefu katika kuhakikisha linapata mafanikio mazuri kama yalivyo kua makongamano manne yaliyo pita, ambayo mawili yalifanyika katika mji wa Laknau na lingine katika mji wa Haidar-abad na la nne katika mji wa Bankaluur.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: