Ataba tukufu za Iraq zashiriki katika furaha za waumini wa India katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Amirulmu-umina (a.s)..

Maoni katika picha
Kutokana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ali (a.s) ambayo inaadhimishwa dunia nzima mashariki na magharibi ikiwa ni pamoja na nchi ya India katika mji wa Kalkata, ambao ni mwenyeji wa kongamano la Amirulmu-uminina (a.s) la kitamaduni awamu ya tano, ambalo linafanyika pamoja na wageni wa Ataba tukufu za Iraq (Atabatu Alawiyya, Husseiniyya na Askariyya) ikiwemo na Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo ndio msimamizi mkuu wa kongamano hilo.

Watumishi wa Ataba tukufu walipo kanyaga aridhi ya Kalkata walipokewa na halaiki kubwa kwa mapenzi na bashasha huku wakitabaruku kwao, hiyo ndio hali ya wapenzi wa Ahlulbait (a.s), wana mafungamano ya kudumu na maimamu wao (a.s) na kila mwenye uhusiano wao, kwa ajili ya kuwaridhisha watu wote na kwa kua muda hautoshi kuitikia mialiko ya watu binafsi na taasisi mbalimbali za kidini, kamati ya maandalizi ilipango ugeni ushiriki katika hafla iliyo fanyika ndani ya Husseiniyya kongwe zaidi, ambayo kongamano pia litafanyika humo Husseiniyya ya utukufu wa mwanamke (Husseiniyya Fadhlu Nisaai) jioni ya siku tukufu ya kuzaliwa kwa imamu Ali (a.s), husseiniyya ilijaa watu na njia yote inayo elekea katika husseiniyya hiyo ilijaa watu waliokua wakisema maneno mazuri mazuri ya makaribisho.

Ugeni ulipita kwa shida kutokana na kufurika kwa watu hadi wakafika katika Husseiniyya hiyo, hafla ilinguliwa kwa maneno ya ukaribisho wa wageni yaliyo semwa na imamu wa husseiniyya hiyo kwaniaba ya waumini wa eneo hilo, Sayyid Ihsaan Jawaad, aliwakaribisha na kuwashukuru pamoja na kuwapa pole ya uchovu wa safari, na akampongeza kila aliye shiriki katika furaha ya kuzaliwa kwa Imamul Muttaqina Ali (a.s), akabainisha kua: “Hakika sisi hua tuna adhimisha mnasaba huu kila mwaka lakini mwaka huu ni tofauti sana kwa kuhudhuria nyuso hizi tukufu”. Akatoa wito kwa wenyeji wanufaike na wageni hao katika muda watakao kaa hapa.

Baada yake aliongea muheshimiwa Sayyid Kadhim Mussawiy ambae ni imamu wa jamaa katika Atabatu Askariyya tukufu, aliwapongeza kwa kushiriki katika mnasaba huu, na akawashukuru kutokana na uzuri wa mapokezi yao ambayo yanaonyesha wazi ukubwa wa mafungamano yao na maimamu wao (a.s), akamuomba Mwenyezi Mungu kwa baraka ya mnasaba huu atuwafikishe kuwatumikia na kufanya kila jambo lenye manufaa.

Kisha akaongea Shekh Ali Fatalawiy ambae ni rais wa kitengo cha elimu na utamaduni cha Atabatu Husseiniyya tukufu, alizungumzia mambo mawili muhimu, kwanza: Alizungumzia utukufu wa Amirulmu-uminina Ali (a.s), pili: Ukaribu na usaidizi wa imamu (a.s) kwa wapenzi wake katika kila sehemu ya dunia, hazuiliwi na sehemu wala muda, akataja hadithi tukufu zinazo fafanua swala hilo.

Akahitimisha maongezi Shekh Mustwafa Abuu Twaabiq rais wa kitengo cha dini katika Atabatu Alawiyya tukufu, akaelezea nafasi na heshima kubwa ambayo Mwenyezi Mungu alimpa imamu Ali na bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Ugeni ukaagwa kama ulivyo pokelewa kwa maneno mazuri na qaswida za wilaya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: