Tarehe kumi na tano ya mwezi wa Rajabu Aswabu hurejea upya huzuni za waumini kwa kufariki mama wa misiba bibi Zainabu (a.s)..

Maoni katika picha
Siku ya kesho tarehe kumi na tano mwezi wa Rajabu ni siku ya huzuni kubwa kwa waumini na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) duniani kote, ni siku aliyo fariki jabali wa subira mama wa misiba bibi Zainabu (a.s), aliondoka duniani na kupumzika kutokana na misiba aliyo pata kwa muda mrefu, akaacha jina lake limeandikwa kwa herufi za nuru katika orodha ya wanawake mashujaa duniani, wanahistoria wametofautiana kuhusu mwaka wa kufariki kwake (a.s), japo kua kauli yenye nguvu kwa wengi ni isemayo kua alifariki mwaka wa (62h), na wengine wanasema alifariki mwaka wa (65h).

Bibi Zainabu (a.s) alisoma kwa baba yake na ndugu zake, na alilelewa katika nyumba tukufu ya Alawiyya, alikua ni mwanamke wa pili kwa utukufu katika watu wa nyumba ya mtume Muhammad (s.a.w.w), uhai wake ulijaa utukufu na karama, alikua ni a’alimu asiye fundishwa, alikua na akili ya hali ya juu kabisa, katika ufaswaha, zuhudi, na ibada zake alikua kama baba yake Amirulmu-uminina na mama yake Zaharaa (a.s).

Bibi Zainab (a.s) alisifika kwa mambo mengi, alijulikana kwa wingi wa tahajudi (swala za usiku), katika hilo alikua sawa na babu yake Mtume (s.a.w.w) na Ahlulbait wengine (a.s), imepokewa kutoka kwa imamu Zainul-abidina (a.s) anasema: (Sikuwahi kumuona shangazi yangu akiswali sunna za usiku akiwa amekaa ispokua siku ya kumi na moja) akikusudia kua hakuacha kuswali sunna za usiku hata siku ile ya huzuni ya kuuliwa kwa kaka yake imamu Hussein (a.s), pindi imamu alipo aga familia yake siku ya Ashura neno la mwisho alilo muambia dada yake alisema: (Ewe dada yangu usinisahau katika sunna zako za usiku).

Bibi Zainab (a.s) katika tukio la Twafu alikua na nafasi muhimu sana, alikua muuguzi wa wagonjwa na hapo hapo alikua anafatilia hatua za kaka yake Hussein (a.s) kila muda, na alikua akimuuliza katika kila tukio, alisimamia mambo yote ya familia, watoto, mayatima na walio elemewa na safari, na ndiye aliye muhami Zainul-abidina alipotaka kuuliwa na ibun Zayadi, akamuambia ibun Ziyadi maneno makali yaliyo mrejesha nyuma, ndiye aliye kimbiliwa na Fatuma mdogo pale alipo sema muovu wa Sham kumuambia Yazidi nipe mimi huyu mateka, bibi Zainabu akamueleza maneno makali Yazidia kama alivyo mueleza ibun Zuyadi.

Ameitwa mama wa misiba, ni haki aitwe hivyo; alishuhudia msiba wa kufiwa na babu yake Mtume (s.a.w.w), na msiba wa kufiwa na mama yake Zaharaa (a.s) pamoja na mitihani aliyo pata mama yake, na msiba wa kuuliwa kwa baba yake Amirulmu-uminina (a.s) na msiba wa kufiwa na kaka yake Hassan (a.s) kwa sumu, na msiba mkubwa wa kuuliwa kwa kaka yake Hussein (a.s) kuanzia mwanzo hadi mwisho, na kuuliwa kwa watoto wake Aun na Muhammad, halafu wakachukuliwa mateka kutoka Karbala hadi Kufa kwa ibun Ziyadi, akaingizwa katika majlisi ya wanaume, wakampokea kwa maneno ya kejeli yanayo choma moyo, kisha wakaondolewa Kufa na kupelekwa Sham huku kichwa cha kaka yake na vya watoto wake pamoja na watu wa familia yake vikiwa vimetungikwa juu ya mikuki mbele ya macho yake njia nzima, hadi wakafika Damaskas wakiwa katika hali hiyo, akaingizwa kwa Yazidi katika majlisi (kikao) cha wanaume…

Amani iwe juu yako ewe bibi yangu, ewe mama wa misiba Zainabu mkubwa, siku uliyo zaliwa na siku uliyo elekea kwa Mola wako ukiwa umeridhia na umeridhiwa na siku utakayo fufuliwa na kua hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: