Kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha mama wa misiba bibi Zainabu (a.s): Atabatu Abbasiyya yafanya mailis ya maombolezo kwa watumishi wake..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba zake za maombolezo ya kuhuisha kifo cha jabali ya subira mama wa misiba bibi Zainabu (a.s) Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Alkhamisi (15 Rajabu 1438 h) sawa na (13 April 2017 m) wamefanya majlis ya maombolezo kwa watumishi wake katika ukumbi wa utawala ndani ya haram tukufu.

Majlis ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watumishi, ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na Amru Alaa Alkifaai, kisha Sayyid Adnaan Jalukhaan Mussawiy kutoka katika kitengo cha dini akatoa muhadhara wa kidini, akaelezea nafasi kubwa aliyokua nayo bibi Zainabu (a.s) katika tukio la Twafu, na namna alivyo simama imara mbele ya Yazidi na mambo yake ya kidhalimu, na namna alivyokua na nafasi ya pekee katika swala hilo, alikua na nafasi ya pili baada ya kaka yake imamu Hussein (a.s), kama tunavyo ona; ndiye aliye angoza msafara baada ya kuuliwa kaka yake, hakika yeye ni japali ya subira, kuna riwaya inasema kua: Hakika Hauraa (Zainabu) (a.s) wakati alipouliwa imamu Hussein (a.s) alienda akamshika mgongoni na akanyanyua mwili wa kaka yake huku akisema: (Ewe Mwenyezi Mungu tukubalie jambo hili), katika mazingira magumu hayo anatafuta radhi za Mwenyezi Mungu, hajawahi kutofautiana na mafundisho ya Mwenyezi Mungu. Majlis ilihitimishwa kwa Qaswida za maomboleza zilizo huisha majonzi ya tukio la kufariki kwake (a.s).

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalumu ya kuomboleza kifo chake (a.s) yenye vipengele vingi vya maombolezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: