Balozi wa Holand Nchini Iraq atembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na akagua miradi yake..

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa watu wanao tembelea Atabatu Abbasiyya tukufu ni wageni wa kidini, kitamaduni na kisiasa. Balozi wa Holandi Nchini Iraq jana siku ya Juma Tano (14 Rajabu 1438 h) sawa na (12 April 2017 m) alitembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, alipokelewa na jopo la viongozi wakiongozwa na katibu wao mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) katika ukumbi wa utawala ndani ya haram tukufu, walijadiliana kuhusu kujenga mahusiano na kusaidiana baina ya miji miwili.

Baada ya hapo balozi alitembea katika korido za Ataba na kukagua miradi yake, miongoni mwa miradi aliyo kaguliwa ni; mradi wa kupauliwa kwa haram, mtambo wa mawasiliano, kamera za ulinzi na makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale.

Mtandao wa Alkafeel ulikutana na balozi wa Holandi na alikua na haya ya kusema: “Nikiwa kama balozi wa Iraq ilikua inanipasa kutembelea kikoa ya Iraq na hasa mji wa Karbala tukufu, kutokana na umuhimu wake kidini na hadhi kubwa uliyo nayo kwa ambapo huja watu kuutembelea kutoka kila kona ya dunia, hakika ni fursa kubwa sana kuutembelea mji ambao unamizizi ya historia ya dini, ziara hii inalenga kuongeza uhusiano na kusaidiana baina ya Nchi mbili Holandi na Iraq hasa katika sekta ya kilimo, nimetembelea mkoa wa Karbala na kuzungumza na viongozi wa mkoa pamoja na viongozi wa chuo kikuu cha Karbala na sasa hivi nipo katika wenyezi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na nimekutana na katibu mkuu na tumeongelea kuhusu kusaidiana”.

Akabainisha kua: “Tumetembelea maeneo ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kukagua mradi wa upauaji wa haram na mtambo wa mawasiliano pamoja na mtambo wa mawasiliano na kamera za ulinzi, hakika imetengenezwa kwa ufanisi mkubwa, halafu tukatembelea makumbusho ya vifaa na nakala kale, kwa hakika tumefurahishwa sana na mpangilio mzuri na namna vifaa vinavyo onyeshwa kwa njia za kisasa kabisa, pia tumevutiwa na vifaa vilivyopo ambavyo ni nadra kuviona katika makumbusho zingine, kuhusu mazingira ya Iraq, hakika tunahisi furaha kubwa na tunaona Daesh wanamalizwa katika nchi ya Iraq chini ya wairaq wenyewe, na tunawaombea utulivu na amani, mwisho tunatoa shukrani kubwa kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mapokezi mazuri waliyo tupatia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: