Ilipo tangazwa kupandisha bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika sehemu inayo fanana na malalo ya imamu Hussein (a.s) katika husseiniyya ya (Fadhlu Nnisaai) ndani ya mji wa Kalkata India, ambayo ni mwenyeji wa kongamano la Amirulmu-uminina (a.s) awamu ya tano, watu walifurika sana kushuhudia tukio hilo, kwa nini isiwe hivyo wakati ni bendera ya kubba tukufu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mtu asiye kua na mipaka ya kieneo wala muda, mapenzi juu yake yameenea kwa watu wote, waandishi wa vitabu, washairi hadi kafikia kilele cha kupendwa kwa hali isiyo kua na mfano.
Wapenzi wa Ahlulbait (a.s) walimiminika kwa wingi katika husseiniyya baada ya kufahamu kuhusu upandishaji wa bendera, kutokana na heshima ya bendera hiyo katika nyoyo za waumini.
Walipo iona na kuyaona maandishi yaliyo andikwa: Ewe mwezi wa bani Hashim (Yaa qamaru bani Hashim) zilisikika sauti za vilio kwa wapenzi wake kutokana na hisia za yaliyo mkuta pamoja na shauku ya kutaka kwenda kufanya ziara katika kaburi lake lililopo katika mji wa Karbala tukufu, ikarejesha katika fikra zao matukio ya bendera katika siku ya Ashura, matukio yanayo umiza nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s).
Sayyid Mukhtaaru Hussein Zaidiy mmoja wa viongozi wa Husseiniyya alisema kua: “Hakika hili ni tukio la kihistoria katika husseiniyya ya (Fadhlu Nisaai), husseiniyya hii tangu ijengwe ina miaka zaidi ya (150) ndio husseiniyya kongwe zaidi katika mji wa Kalkata, na kwa utukufu wa bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi imekua takatifu zaidi.
Jicho la mtandao wa Alkafeel lilikuwepo katika shughuli hiyo na limekuletea picha za tukio hilo tukufu, tukio ambalo wahudhuriaji walionyesha kulifurahia sana.