Ufunguzi wa hospitali ya Amirulmu-uminina (a.s) katika mkoa wa Najafu Ashrafu..

Maoni katika picha
Ofisi ya Mheshimiwa Marjaa dini mkuu Sayyid Ally Hussein Sistani (d.dh.w) katika mji wa Najafu Ashrafu siku ya Juma Tano (14 Rajabu 1438 h) sawa na (12 April 2017 m) wamefanya ufunguzi wa Hospitali ya Rufaa Amirulmu-uminina (a.s) iliyo jengwa na kusimamiwa na ofisi yake tukufu, ufunguzi huu unafatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Amirulmu-uminina (a.s), na inalenga kusaidia mafukara na watu wasio kua na uwezo, itatoa huduma kwa gharama nafuu zaidi kwa ajili ya kulipa huduma za uendeshaji tu, bila kupata faida hata kidogo ya kiuchumi..

Katika ufunguzi huo alihudhuria kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i) na Muhandisi Sayyid Muhammad Ashiqar katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na jopo kubwa la viongozi wenzake watukufu, hali kadhalika kulikua na mahudhurio makubwa ya maulamaa pamoja na wawakilishi wa Maraajii wengine watukufu (d.dh) pamoja na walimu wa hauza na wakazi wa mji mtukufu wa Najafu.

Kamati iliyo simamia mradi ilisema kua: “Hospitali ya Amirulmu-uminina (a.s) iliyopo katika mtaa wa Swiha karibu na mahakama ya mwanzo ya Najafu Ashrafu imejengwa kwa amri na maelekezo ya Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani (d.dh.w), nayo imejikita zaidi katika matibabu ya macho, moyo, na upasuaji kwa ujumla, ina vitanda (200), imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa (2,250 m2) ina ghorofa saba pamoja na kumbi za kuelekea kwa madaktari na vyumba sita vya upasuaji vilivyo na vifaa tiba vya kisasa zaidi, vyumba vitatu ni maalumu kwa upasuaji (opretion) za macho na vitatu vingine kwa upasuaji wa aina zingine”.

Wakaongeza kusema kua: “Hospitali hii inatuma ujumbe kwa walimwengu kua Iraq bado ipo imara, itaendelea kuishi na inaendeleza ujenzi pamoja na mazingira magumu inayo pitia kutokana na mashambulizi makali kutoka kwa magenge ya kigaidi na vibaraka wao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: