Kupiga kura ya kuwapata washindi katika kongamano la Amirulmu-uminina (a.s) wakazi wa mji wa Kalkata nao ni miongoni mwa washindi..

Maoni katika picha
Jioni ya Ijumaa (16 Rajabu 1438 h) sawa na (14 April 2017 m) ilifanyika kura iliyo husisha kujibu maswali kuhusu historia ya imamu Ali (a.s) ambayo ilikua ni miongoni mwa ratiba za kongamano la Amirulmu-uminina (a.s) la kitamaduni awamu ya tano, shindano hili la kujibu maswali kisha kuingia katika hatua ya kupigiwa kura ni miongoni mwa ratiba muhimu sana na ambayo huvutia watu wengi, kwa sababu zawadi yake inathamani zaidi kwa raia wa nchi hii wafuasi wa Ahlulbait (a.s), ambayo ni kuzuru Ataba tukufu za Iraq, na ndio ndoto ya watu wengi.

Kamati ya maandalizi imetenga nafasi za washindi (20) watakao gharamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu safari za kwenda na kurudi Iraq pamoja na kutembelea Ataba mbalimbali za huko na mazaru tukufu, nayo Atabatu Husseiniyya tukufu imejitolea kugharamia watu watano hivyo jumla kuna nafasi ya watu (25) watakao gharamiwa safari za kwenda kufanya ziara nchini Iraq. Watapatikana kwa kujibu maswali yanayo ulizwa katika siku zote za kongamano, walio jibu sahihi ndio watakao pigiwa kura ili kuwapata watu ishirini na tano.

Jambo la kuzingatiwa hapa, furaha za washindi ni sawa na furaha za walio shindwa au hata wale ambao hawakushiriki kabisa, utaona watu wote wanafurahia, wao husema: “Hakika sisi ni washindi pia, kwa sababu mji wa Kalkata umepata utukufu wa kuwakaribisha watumishi wa Ataba tukufu, kwa kuwepo wao katika mji huu na kwa baraka zao tumeishi maisha mazuri kabisa ya kiroho, halafu watakapo rudi wao na hawa walio shinda watatufanyia ziara kwa niaba na kutuombea dua”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: