Kiongozi wa tabligh katika Atabatu Abbasiyya tukufu aendesha swala ya Ijumaa katika msikiti uliojengwa na muiraq kabla ya karne huko India..

Maoni katika picha
Masjid (Albasrawiy) kama unavyo itwa na wakazi wa mji wa kihistoria wa Kalkata India, hilo ndio jina lake rasmi, mtandao wa Alkafeel ulikuwepo wakati imamu wa msikiti huo alipo toa mwaliko wa kuhudhuria kongamano la Amirulmu-uminina (a.s) kwa wageni wa Ataba tukufu na kuwaomba swala ya Ijumaa iongozwe na mmoja wao.

Hivyo swala ya Ijumaa iliongozwa na Shekh Asadiy ambaye ni kiongozi wa tabligh katika Atabatu Abbasiyya tukufu, swala ilihudhuriwa na mamia ya waumini, Shekh Asadiy alitoa hotuba mbili kwa lugha ya kiarabu, katika hotuba ya kwanza alizungumzia utukufu wa Amirulmu-uminina (a.s) na umuhimu wa kufuata mwenendo wake, alitaja visa kadhaa vya historia ya maisha yake (a.s).

Na katika hotuba ya pili akazungumzia umuhimu wa kufuata mwenendo wa kibinadamu walio kua nao maimamu wa Ahlulbait (a.s) wa kuishi kwa amani na watu wa dini na madhehebu yote, hususan katika nchi yenye dini nyingi mfano wa India, akasisitiza kua wanatakiwa kua mfano bora kwa watu wengine, ili wawalinganie watu katika haki bila kutumia ndimi zao, ambao ndio wasia wa Mtume na Ahlulbait (a.s) kwa waumini.

Pia kulikua na ujumbe elekezi kutoka kwa wageni uliotolewa na kiongozi wa kituo cha turathi za Karbala katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Dokta Ahsaan Ghuraifi baada ya swala, ambaye alihimiza umihimu wa kushikamana na mafundisho ya maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kufuata mwenendo wao mtukufu.

Naye mjukuu wa muasisi wa msikiti huo aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Babu yangu alikuja India akitokea katika mji wa Basra kusini mwa Iraq, akajenga msikiti huu na kua kitovu cha mafundisho ya dini kwa kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s), kwa karne zoto tangu ujengwe msikiti huu umekua makao makuu ya uongofu katika nchi yenye dini nyingi, na leo katika zama za ukarabati wake tumepokea ugeni kutoka katika Ataba tukufu hakika mmeuongezea baraka zaidi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: