Imamu wa Ijumaa katika msikiti wa (Al-basrawiy) India, awazawadia viongozi wa ugeni wa Ataba tukufu wanao shiriki katika kongamano la Amirulmu-uminina (a.s) la kitamaduni..

Maoni katika picha
Sayyid At-haru Abbasi ambaye ni imamu wa Ijumaa na swala za jamaa katika msikiti wa Albasrawiy nchini India, amewazawadia viongozi wa ujumbe wa Ataba tukufu (Atabatu Alawiyya, Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya) waliokuja kushiriki katika kongamano la Amirulmu-uminina (a.s) la kitamaduni awamu ya tano lililo maliza hatua yake ya kwanza hapo jana katika husseiniya ya Fadhlu Nisaai ndani ya mji wa Kalkata.

Lilifanyika hilo baada ya ugeni huo kukubali mwaliko wake wa kushiriki katika hafla ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s), mji unaendelea kuishi katika harufu ya kumbukumbu hiyo kwa kufanyika majlis na hafla mbalimbali, ikiwemo hafla hii iliyokua na mahudhurio makubwa sana ya wakazi wa mji huu na miji ya jirani yake, watu walimiminika kwa wingi katika msikiti huo baada ya kusikia kua kutakua na wageni kutoka katika Ataba tukufu za Iraq.

Zawadi walizo pewa Ataba tukufu ni kifaa cha Fedha kitakacho ingizwa katika vifaa vya Ataba na mikufu ya maua, Sayyid At-haru Abbasi Ridhawiy aliongea maneno ya ukaribisho wa wageni kisha rais wa wageni wa Ataba tukufu Shekh Mustwafa Abuu Twabuuq akaongea kwaniaba ya wageni, akaelezea baadhi ya utukufu wa Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s), akawataka washiriki washikamane na mwenendo wa imamu Ali (a.s), halafu wageni wa Ataba wakasimama na kugawa zawadi za tabaruku kwa wahudhuriaji wa hafla hiyo.

Mjukuu wa muasisi wa msikiti huo aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Babu yangu alikuja India akitokea katika mji wa Basra kusini mwa Iraq, akajenga msikiti huu na kua kitovu cha mafundisho ya dini kwa kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s), kwa karne zoto tangu ujengwe msikiti huu umekua makao makuu ya uongofu katika nchi yenye dini nyingi, na leo katika zama za ukarabati wake tumepokea ugeni kutoka katika Ataba tukufu hakika mmeuongezea baraka zaidi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: