Shekh Fatalawiy: Utukufu wa Amirulmu-uminina (a.s) hauwezi kufananishwa na alimu mkubwa wala khatwibu faswaha wala muandishi mahiri kwa sababu hakuna anaemjua ispokua Mwenyezi Mungu na mtume wake..

Maoni katika picha
Hakika utukufu wa Amirulmu-uminina (a.s) hauwezi kufananishwa na alimu mkubwa wala khatwibu mfaswaha wala muandishi mahiri kwa sababu hakuna anaemjua ispokua Mwenyezi Mungu na mtume wake.. haya yalisemwa na Shekh Ali Fatalawiy muwakilishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu katika khutuba aliyo toa kwaniaba ya ugeni wa Ataba tukufu katika kuhitimisha kongamano la Amirulmu-uminina (a.s) la kitamaduni awamu ya tano ambalo sehemu yake ya pili itaendelea katika mji wa Binghali magharibi ya India.

Akaongeza kusema kua: “Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu aliye tuneemesha kukutana na nyie na akaturuzuku kuwatumikia, na tunakupongezeni kwa kuzaliwa hoja tukufu na habari kubwa simba wa Mwenyezi Mungu mwenye kushinda Ali bun Abuutwalib (a.s)”.

Kisha Shekh Fatalawiy akasoma hadithi zinazo elezea utukufu na ubora wa imamu Ali (a.s) miongoni mwa hadithi hizo ni:

Kwanza: katika uumbwaji wake, anasema mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): “Mimi na Ali tulikua nuru kwa Mwenyezi Mungu kabla ya kuumbwa Adam kwa miaka elfu kumi na nne, alipo umbwa Adam nuru ile ikagawiwa sehemu mbili; sehemu yangu na sehemu ya Ali”.

Pili: Kuhusu kumtii, amesema mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): “Atakaye nitii atakua amemtii Mwenyezi Mungu na atakaye niasi atakua amemuasi Mwenyezi Mungu, na atakaye mtii Ali atakua amenitii mimi na atakaye muasi Ali atakua ameniasi mimi”

Tatu: Kuhusu kumfuata, anasema mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): “Namuusia kila aliye niamini na kunisadikisha amtawalishe Ali bun Abuutwalib, atakaye mtawalisha atakua amenitawalisha mimi, na mwenye kunitawalisha mimi atakua amemtawalisha Mwenyezi Mungu mtukufu, na mwenye kumpenda atakua amenipenda mimi, na mwenye kunipenda mimi atakua amempenda Mwenyezi Mungu, atakaye mchukia atakua kanichukia mimi na mwenye kunichukia mimi atakaa amemchukia Mwenyezi Mungu”.

Nne: Ni bishara njema kwenu, anasema mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): “Ewe Ali hakika Mwenyezi Mungu amekusamehe wewe na familia yako na watoto wako na watu wako na wafuasi wako na watakao wapenda wafuasi wako nakubashiria hakika wewe ni muokoaji”.

Shekh Fatalawiy akamalizia kwa kusema: “Natoa shukrani kwa kila aliye changia kufanikisha jambo hili tukufu, na ninamuomba Mwenyezi Mungu atujalie kua miongoni mwa watakao fuata mwenendo wa Ali (a.s)”
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: