Kwa kusimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kitengo cha malezi na elimu ya juu wamefanya hafla ya kufikisha miaka ya kuwajibikiwa na sheria (kubalehe) kwa wanafunzi wa shule za Abulfadhil Abbasi (a.s), ndani ya ukumbi wa jengo la shekh Kuleiniy (q.s), lililo chini ya Ataba tukufu katika barabara ya (Bagdadi – Karbala), hafla hiyo iliyo dumu siku mbili ilihusisha kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za (Al-ameed na Alqamaru shule za msingi za wasichana) na wanafunzi wa shule ya upili (sekondari) ya (Sayyid Almaau ya wavulana), zawadi hizo zimetolewa na Ataba tukufu kwa lengo la kuwafanya wahisi umuhimu wa hatua ya umri wanayo ingia pamoja na majukumu na wajibu wao kisheria.
Hafla ilihudhuriwa na idadi kubwa ya viongozi wa Ataba tukufu, pamoja na idadi kubwa ya wanafunzi na wazazi/walezi wao, ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaibwa wimbo wa taifa na wimbo wa Ataba tukufu.
Kisha rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu dokta Abbasi Mussawiy akaongea, miongoni mwa aliyosema ni: “Hakika kazi ya malezi na kusomesha haiishii katika ukumbi wa darasa peke yake, bali kumbi za darasa ni sehemu ndogo miongoni mwa sehemu ambazo zinamjenda mwanafunzi katika nyanja tofauti, kitengo cha malezi na elimu ya juu kinatambua hilo, hivyo kimeandaa nidhamu ya kiislamu kwa kufuata mitazamo ya kimataifa na kuishauri Ataba tukufu kuendesha ratiba ya wazi na yenye manufaa makubwa kimalezi na kielimu”.
Akaongeza kusema kua: “Miongoni mwa ratiba za kimalezi zinazo saidia kuwajenga wanafunzi kiroho ni hafla za kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria (kubalehe), hutolewa mawaidha elekezi katika hafla hizo pamoja na zawadi ambazo huchangia sana kuwajenga kiroho, huendelea kufundishwa mabadiliko yanayo tokea katika maisha yao kidogo kidogo ili kuwaandaa kiroho kuingia katika hatua ya kuwajibikiwa na sheria, na kuwafanya wafahamu kua sasa wanaingia moja kwa moja katika walengwa anao wakusudia Mwenyezi Mungu pale alipo sema: (Na wala sikuwaumba majini na binadamu ispokua waniabudu mimi)”.
Akafafanua kua: “Hakika ratiba hii ya makuzi, ni moja ya ratiba za malezi zinazo simamiwa na kitengo chetu moja kwa moja katika sekta ya malezi”.
Hafla hii iliyo dumu siku mbili ilikua na mambo mengi yaliyo fanywa na vijana wanao ingia katika umri wa kuwajibikiwa na sheria, siku ya kwanza ambayo ilikua maalumu kwa wasichana waliimba tenzi nyingi zilizo kua na anuani isemayo (Kuwajibikiwa kwangu kunatoka kwa Mola wangu), kisha walikua wakirejea rejea kiapo kitukufu (kiapo cha kuwajibikiwa na sheria), pia walifanya igizo lililo onyesha kuhusu vazi la hijabu na jinsi alivyo kua bibi Fatuma Zaharaa (a.s), na igizo lingine lilihusu (matawi ya dini), pia walipewa zawadi ambazo ni vitu anatakiwa kuvitumia mtu anaewajibikiwa na sheria kila siku ambavyo ni: (Hijabu, Mswala, Turba, Tasbihi na Qur’an tukufu).
Siku ya pili wanafunzi wanao ingia katika umri wa kuwajibikiwa na sheria (kubalehe) walifanya maigizo matatu, igizo la kwanza lilikua na anuani isemayo: (Mitandao ya mawasiliano na athari zake kwa jamii), na igizo la pili lilihusu ushujaa wa Hashdi Sha’abi dhidi ya magaidi ya Daesh, huku igizo la tatu likihusu imamu wetu wa zama, imamu Mahadi (a.f), na mwisho wa hafla zilitolewa zawadi kwa wanafunzi wanao ingia umri wa kuwajibikiwa na sheria baada ya kusoma kiapo cha kuwajibikiwa na sheria, pia katika hafla hiyo; kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na taasisi ya Nurul Hassan (a.s) pamoja na taasisi ya Alkafeel walitoa msaada kwa shule washiriki.