Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu atembelea miradi ya Ataba akifuatana na spika wa bunge la mkoa wa Karbala pamoja na baadhi ya wabunge..

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) na jopo la viongozi wa Ataba tukufu wakiongozana na spika wa bunge la mkoa wa Karbala siku ya Juma Pili (18 Rajabu 1438 h) sawa na (16 April 2017 m) wametembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, iliyo kamilika na mambayo bato ipo katika hatua ya utekelezaji, miongoni mwa sehemu walizo tembelea ni shule ya msingi Alqamar ya wasichana iliyo funguliwa hivi karibuni, pamoja na miradi ya magodauni na majengo ya shule hali kadhalika walitembelea karakana ya Alkafeel, wageni walionyesha kufurahishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hii pia maendeleo makubwa yaliyo fikiwa.

Ili kufahamu zaidi kuhusu matembezi hayo, rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi Ustadhi Dhiyaau Majidi aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Miongoni mwa mapendekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) ni kuwajulisha wakazi watukufu na viongozi wa serikali mafanikio na miradi ya kijamii inayo fanywa na Ataba tukufu, hivyo matembezi aliyo fanya Sayyid Muhammad Ashiqar (d.i) akifuatana na spika pamoja na wabunge wa bunge la mkoa wa Karbala na kutembelea shule ya Alqamar iliyo chini ya Ataba tukufu, na kukagua vitengo vyake pamoja na kiwango cha elimu inayo tolewa, baada ya hapo tukaenda katika miradi mingine, ambayo ni mradi wa godauni na majengo ya shule, na sehemu za michezo ya watoto, baada ya hapo tukaelekea katika karakana ya Alkafeel halafu tukatembelea miradi ya vifaa vya kilimo, mfano kiwanda cha mbolea na vinginevyo, pia tukatembelea majengo ya Alkafeel, na tukamaliza matembezi yetu kwa kutembelea vitalu vya Ataba tukufu, wageni walionyesha kufurahishwa sana na miradi hii”.

Spika wa bunge la mkoa wa Karbala Sayyid Naswifu Jaasim Khatwabi alisema kua: “Sio jambo geni kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kukamilisha miradi mingi na kwa ufanisi mkubwa ndani ya muda mfupi, na manufaa ya miradi hiyo yanarudi kwa jamii na watu wanaokuja kufanya ziara, leo tumetembelea baadhi ya miradi iliyo kamilika na ambayo bato ipo katika utekelezaji, kwa hakika miradi tuliyo tembelea imetekelezwa kwa ufanisi mkubwa, sawa uwe ni mradi wa kielimu, utoaji wa huduma au wa kilimo, nawashukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu na watu woto walio pelekea kukamilika kwa miradi hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: