Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wawatembelea wapiganaji katika mji wa Mosul na wawapa misaada..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu yaendelea na ziara zake za kuwatembelea wapiganaji waliopo katika viwanja vya mapambano toka kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda na Marjaa dini mkuu, kwa ajili ya kuwapa msaada wa kimaanawiyya na kimkakati kwa vikosi vya wapikanaji, ili ziara hizi zidumu watumishi wa kitengo cha habari na utamaduni wameunda kikundi na kukipa jina la (kwa ajili yenu) kazi yao ni kutembelea vikosi vya wapiganaji waliopo ndani ya viwanja vya mapambano katika mji wa Mosul na kuwapa misaada.

Ziara hii iliyo fanywa kwa ushirikiano na vitengo vingine vya Ataba tukufu, imefanyika baada ya kukusanya michango kutoka kwa watumishi ambao walionyesha mwitikio mkubwa, kutokana na michango hiyo; tulinunu nafaka za chakula, juis na mifuko ya unga, vikafungwa na kugawiwa kwa vikosi vya wapiganaji kwa mtindo wa kapu (furushi) la chakula, pia waligawa nakala za misahafu na baadhi ya vitu vingine vya kutabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pia ziliandaliwa nafaka zingine za chakula kwa ajili ya kuwapa wakimbizi wa mji wa Mosul.

Ziara ilichukua siku mbili na tulifanikisha kuwatembelea: kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, Liwaau Answaru Marji’iyya na kikosi cha Alfajru pamoja na vikosi vingine vilivyopo katika miji ya Badushi, Tal-faris, Hamaamul-alil na Tal-abatwa, miji yote hiyo ilikombolewa kwa juhudi za wapiganaji hao mashujaa.

Tunapenda kusema kua Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea kutuma misafara ya kutoa misaada kwa vikosi vya wapiganaji waliopo katika viwanja vya mapambano toka ilipo tolewa fatwa tukufu ya kujilinda na Marjaa dini mkuu hadi leo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: