Kwa ajili ya kuboresha kiwango cha elimu cha wanafunzi: kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu chafanya maonyesho..

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu jana siku ya (19 Rajabu 1438 h) sawa na (17 April 2017 m) kimefanya maonyesho ya vifaa vya kufundishia katika shule za Ameed, maonyesho haya yaliyo fanyika katika shule ya msingi ya Saaqi yamehusisha vifaa vya kufundishia zaidi ya (64), vinavyo saidia kuongeza kiwango cha elimu na kutoka katika hatua ya nadhariyya na kuingia katika utendaji.

Hafla ya ufunguzi wa maonyesho hayo ilipata muitikio mkubwa, na ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu wa Iraq, halafu ukafuata ujumbe wa kitengo cha malezi na elimu ya juu ulio tolewa na rais wa kitengo hicho dokta Abbasi Mussawiy, alisema kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu imejitahidi kuweka utaratibu wa masomo unao endana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu (d.dh) na imefanikiwa kufungua taasisi taasisi mbalimbali na shule, miongoni mwa mambo mazuri ya utaratibu huo, ni kwamba; haitoshi kupata elimu kwa kukaa darasani peke yake, bali kukaa darasani ni moja kati ya njia za kutafuta elimu, kwa kuzingatia hilo kitengo cha malezi na elimu ya juu kimeufanyia kazi mtazamo huo na kuandaa vifaa saidizi vya kujifundishia”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika kitengo cha malezi na elimu ya juu kimeandaa vifaa saidizi vya kufundishia, baadhi ya vifaa hivyo kwa miaka mingi vilikua havipewi umuhimu wowote, pia tumefanya juhudi ya kutengeneza vifaa saidizi vya kufundishia ambavyo vinasaidia akili kuelewa masomo kwa urahisi zaidi, kwa sababu mwanafunzi huelewa zaidi masomo kwa kutumia vitendo kuliko nadhariyya”.

Hafla ilipambwa na mambo kadhaa yaliyo fanywa na wanafunzi, kisha wahudhuriaji walielekea katika ufunguzi rasmi wa maonyesho ya vifaa saidizi vya kufundishia vilivyo shiriki katika maonyesho hayo yaliyo husisha zaidi ya vifaa (64).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: