Kwa lengo la kubadilishana uzowefu wa kitabibu: hospitali ya rufaa Alkafeel yasaini mkataba na wizara ya afya ya Bilaroos..

Maoni katika picha
Kutokana na kuendelea kuboresha huduma za matibabu, hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imesaini mkataba na wizara ya afya ya Bilaroos unao husu mafunzo ya utoaji wa huduma za kitabibu, mkataba huo unalengo la kubadilishana uzoefu na kujenga uwezo kwa ajili ya kutoa huduma bora zaidi kwa wagonjwa, pia wamekubaliana kufanya biashara ya dawa na vifaa tiba na kusaidiana katika utengenezaji wake.

Makubaliano haya yamefikiwa baada ya waziri wa Bilaroos kutembelea hospitali ya Alkafeel na kuona maendeleo yake. Ambapo waziri huyo na ugeni alio ongozana nao waliridhishwa na vifaa tiba vinavyo milikiwa na hospitali hii pamoja na huduma inayo tolewa kwa wagonjwa.

Kiongozi mkuu wa hospitali Dokta Haidari Bahadeli aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kutokana na mwaliko rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ugeni kutoka nchi ya Bilaroos wametembelea hospitali ya rufaa Alkafeel kwa lengo la kukagua hatua ya maendeleo iliyo piga katika utoaji wa huduma za tiba, ugeni huo ukiongozwa na waziri wa afya; alifuatana na jopo la madaktari bingwa wa maradhi mbalimbali pamoja na viongozi wa makanpuni yanayo tengeneza dawa na vifaa tiba”.

Akabainisha kua: “Katika ziara hii tumesaini mkataba wa ushirikiano kwa lengo la kuongeza ubora zaidi katika utoaji wa huduma za tiba kwa wagonjwa, kutokana na mkataba huu; hospitali ya Alkafeel itapokea jopo la madaktari bingwa wa maradhi mbalimbali kutoka Bilaroos watakao shiriki katika kazi za upasuaji ndani ya hospitali hii na kubadilishana uzoefu, mkataba huu utakua ni mwanzo mwema wenye manufaa baina yetu”.

Akaongeza kusema kua: “Wizara ya afya ya Bilaroos itatoa ushirikiano mkubwa katika kutatua kesi mbalimbali za kitabibu na kuhamisha uzoefu wao wa kitabibu hapa Iraq”.

Akasema kua: “Tumekubaliana na Bilaroos kushirikiana katika sekta ya kutengeneza dawa hapo baadae”.

Ugeni wa Bilaroos siku ya Juma Nne (19 Rajabu 1438 h) sawa na (17 April 2017 m) ulitembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na wakatembelea baadhi ya miradi yake na kukagua maendeleo yake pia walitembelea makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: