Hela za sarafu na za noti nadra ni miongoni mwa vitu vilivyopo katika makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale..

Maoni katika picha
Makumbusho ya Alkafeel ina mamia ya hela za sarafu na za noti zilizo wekwa kwa umaridadi mkubwa ili kuwavutia watu wanao tembelea makumbusho hiyo, historia ya hela hizo inarejea katika zama tofauti, kama vile zama za utawala wa Ighriqiyya, Roma, Umawiyya, Abbasiyya, Othmaniyya na zama zingine, baadhi ya hela hizo zilitolewa zawadi na watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na baadhi tulizinunua na kuzikusanya, kwa maelezo zaidi kuhusu hela hizo mtandao wa Alkafeel uliongea na kiongozi wa makumbusho Ustadh Swadiq Laazim, ambaye alisema kua: “Hela za sarafu na za noti huzingatiwa kua miongoni mwa athari muhimu ya kihistoria inayo unganisha baina ya kizazi na tamaduni za kizazi kilicho pita, kupitia michoro inayo patikana katika hela hudhihirisha kiwango cha ufundi wa watu walio zitengeneza na jamii ya wakati huo, hivyo hela ni dalili muhimu ya kihistoria ambayo hudumu karne na karne, kwa sababu hiyo makumbusho nyingi hutilia umuhimu mkubwa wa kuhifadhi hela za zamani ikiwemo makumbusho ya Alkafeel, tulianza kukusanya hela za sarafu na za noti tangu mwaka (2003 m), baadhi yake tulipewa zawadi na watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhili Abbasi (a.s), bado watu wanaendelea kutuletea zawadi ya hela za zamani hadi leo, na baadhi yake tumenunua, hadi sasa tuna zaidi ya sarafu (1,000) ambazo historia yake inarejea katika zama tofauti, kama vile zama za Ighriqiyya, Roma, Sasaniyya, Umawiyya, Abbasiyya, Fatwimiyya, Swafawiyya, Othmaniyya pamoja na hela za noti za wakati wa zama za mfalme wa Iraq”.

Akaongeza kusema kua: “Katika makumbusho hii tumetengeneza sehemu maalimu ya kuzitunza na kuzihifadhi, pamoja na kuweka kumbukumbu zake ambazo ni; aina ya hela, michoro au maandishi yaliyopo katika hela hiyo, ukubwa na uzito wake, sehemu ilipo tengenezwa, mwaka wa kutengenezwa kwake na mengineyo, ili kulifanikisha hili kwa ufanisi mkubwa tulitumia wasomi wa sekula kutoka katika vyuo vikuu vya Iraq pamoja na watu wenye uzoefu wa hela za zamani kwa ajili ya kuzitambua na kubaini uhalisia wake”.

Akabainisha kua: “Kuhusu urekebishaji na utunzaji wa sarafu hizi kuna kitengo maalumu katika makumbusho hii kinacho fanya kazi hiyo baada ya kuwapa kozi maalumu ya namna ya kutunza na kusafisha sarafu za zamani pamoja na kuzingatia kiwango cha joto na baridi katika utunzaji wake, wakati mwingine huzichovya katika dawa kwa ajili ya kuzihifadhi, kutokana na umuhimu wa safafu husika, sarafu ni kielelezo muhimu sana cha kihistoria, miongoni mwa sarafu muhimu tulizo nazo ni ile sarafu ya kiarabu iliyo tumika katika zama za imamu Ridha (a.s).

Kuhusu namna ya uonyeshwaji wake Ustadh Swadiq alisema kua: “Miongoni mwa vitu muhimu katika makumbusho ni namna ya kuonyesha vitu vyake, kwa sababu vinatakiwa vilete mvuto kwa mtu anaye kuja kuitembelea, hakika kulikua na tatizo katika namna ya kuonyesha sarafu, kwanza tuliziweka kwa mtindo wa urefu, tukagundua aina hiyo haikati kiu ya mtu anaye kuja kuitembelea makumbusho kutokana na udogo wa safafu na umuhimu wa maelezo yake, tukabadilisha na kuziweka kwa upana kama mnavyo ziona leo katika makumbusho hii ya Alkafeel, baada ya kuangalia katika makumbusho zingine tulizo tembelea, kama vile makubusho za Ufaransa, Itali na Uturuki, tukaona kua njia bora ya uonyeshaji wa sarafu ni ile tuliyo ikuta katika makumbusho ya Itali, hivyo tukaiga uwekaji wao”.

Akaongeza kusema kua: “Tuna fikra ya kuongeza katika maonyesho ya makumbusho maelezo ya namna ilivyo kua ikitumika kila sarafu, na kazi hiyo inaendelea –inshallah- pamoja na kubainisha mahala na zama iliyo tengenezwa, pia tuna mradi wa kuandaa nakala ya sarafu itakayo tengenezwa kwa plastiki na kuvipa vyuo vikuu na vituo vya kitafiti kwa ajili ya kufundishia mambo yanayo husu sarafu za kale kwa wanafunzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: