Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukifu ukiongozwa na rais wa kitengo cha mahusiano umeshiriki katika hafla ya kubadilisha bendera za maimamu wa Kadhimain (a.s), kwa kuwekwa bendera nyeusi zinazo ashiria huzuni kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya shahada ya imamu Mussa Al-kaadhim (a.s) ambayo kilele chake itakua tarehe 25 Rajabu Aswabu, hafla hiyo imefanyika katika uwanja wa haram tukufu ya Kadhimiyya tarehe 22 Rajabu 1438 h, sawa na 20 April 2017 m.
Katika hafla hii ya maombolezo palitanda huzuni kubwa, katika siku hizi ambazo Ataba tukufu inapokea makundi ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wanaokuja kuhuisha kumbukumbu ya shahada ya imamu wao Mussa Al-kaadhim (a.s), aliye uawa ndani ya jela ya Haruna Rashidi.
Hafla hii ilihudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya tukufu dokta Jamali Abdurasuul Dabagh na jopo la wajumbe wa kamati ya uongozi pamoja na muwakilishi wa Marjaa dini mkuu wa mji wa Kadhimiyya, na walimu wa mradi wa tablighi pamoja na wanafunzi wa hauza, bila kuwasahau wawakilishi wa Ataba tukufu na wawakilishi wa serikiali na kundi kubwa na waumini na wanajamii pamoja na watumishi wa maimamu wawili watukufu (Jawaadain) na vikundi vya maombolezo na watu walikuja kufanya ziara (mazuwaru watukufu).
Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha makundi ya maombolezo ya mji wa Kadhimiyya yalishiriki kwa kuimba qaswida za maombolezo huku wakiwa wamebeba bendera za wilaya katika kuonyesha huzuni ya tukio la kusikitisha, kisha ukafuata ujumbe wa Atabatu Kadhimiyya tukufu ulio wasilishwa na katibu mkuu wa Ataba hiyo dokta Jamali Abdurasuul, miongoni mwa aliyo sema ni: “Shughuli ya kupandisha bendera vyeusi katika kubba za maimamu wawili watukufu (a.s), inatukumbusha kupinga kila aina ya dhulma, bila shaka kinazijenga nyoyo za waumini kua na ujasiri wa kuwapinga madhalimu na kujitenga na vitendo vyao, jambo hilo lipo kimaumbile kutokana na utukufu alio pewa mwanadamu wa kupinga kunyanyaswa na kudhulumiwa katika maisha yake”.
Halafu ukafuata ujumbe wa mradi wa tabligi ulio wasilishwa na muwakilishi wa Marjaa dini mkuu Shekh Hussein Aali-Yaasin, alianza na usia wa imamu Kaadhim (a.s) kwa Hisham bun Hakam unaoelezea wasifu wa imamu (a.s), akaongeza kua: “Marja’iyya tukufu na walimu wa hauza pamoja na wanafunzi wao wanaendelea kuomba dua na kusaidia sekta mbalimbali, sekta ya vita dhidi ya magaidi, sekta ya elimu, sekta ya tablighi na sekta ya huduma za jamii”.
Hafla ilihitimishwa kwa kubadilisha bendera za maimamu wawili watukufu wa Kadhimain huku zikisikika sauti za: (Labaika yaa masmuum) huku muimbaji mashuhuri wa mimbari ya Husseiyya Haaji Baasim Karbalai akiimba qaswida za maombolezo.