Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu chafanya nadwa kuhusu turathi za Hilla..

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo: (Hilla ni msingi wa ubunifu na huisho la utafiti), kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Baabil asubuhi ya Ijumaa (23 Rajabu 1438 h) sawa na (21 April 2017 m) wamefanya nadwa kuhusu turathi za Hilla katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s) ndani ya Ataba tukufu.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukafuatia ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliowasilishwa na rais wa kitengo cha maarifa Shekh Ammaar Hilaliy ambaye alisema: “Hakika turathi za umma ndio kumbukumbu yao na historia yao pia ni mwenendo unaotakiwa kuchukua mazingatio, unaposoma zana na njia walizo tumia kufikia malengo yao, mji wa Hilla una nafasi kubwa katika turathi za kiislamu kutokana na athari za wanazuoni wakubwa wa mji huo, hakika ulikua mji wa maulamaa watukufu ambao mafundisho yao yanafatwa na wanadamu hadi leo, bado kalamu za vizazi na zizazi zinanukuu mafundisho yao matukufu, hafla hii inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Baabil ni sehemu ya kuenzi mafundisho yao matukufu”.

Kisha ukafuata ujumbe wa chuo kikuu cha Baabil ulio wasilishwa na mkuu wa kitivo cha Tarbiya dokta Muhammad Rabii, ambaye alisema kua: “Hilla ni mji wa imamu Hassan (a.s) ni kielelezo cha elimu na utukufu, una turathi nyingi sana, miongoni mwa turathi zake zipo katika maandishi na kuna haja kubwa ya kunufaika nazo, kituo cha turathi za Hilla chini ya Ataba tukufu kinafanyia kazi swala hili, mnafahamu kua chuo kikuu kinaendelea na utafiti wa kielimu kuhusu turathi hizo, hivyo chuo kimejikita katika tafiti za kidini, kifiqhi na kitamaduni katika nyanja zote, ili kubaini turathi zote za kiislamu kuanzia kuchomoza kwa mji wa Hilla kama kituo cha elimu”.

Baada ya hapo kikaanza kikao cha kitafiti kilicho ongozwa na dokta Ali A’arajiy kilicho jadili tafiti nane zifuatazo:

  • 1- Dokta Said Jaasim Zubaidiy, utafuti wake ulihusu: (Muonekano wa uhuishaji wa Nahau kwa mujibu wa Shekh Yusufu Karkushi).
  • 2- Shekh Mithaaq Abbasi Khafajiy, utafiti wake ulihusu: (Misingi ya tafiti za qur’an katika madrasa ya Hilla baina ya karne ya sita na ya saba hijiriyya masomo ya mukaarana, ibun Idrisa aliye fariki (598 hijiriyya) na ibun Twausi aliye fariki (664 hijiriyya) na muhakiki Hilliy aliye fariki (676 hijiriyya) kama mfano).
  • 3- Dokta Haamid Naasir Dhwalimiy, utafiti wake ulihusu: (Abdurahmaan Ataaiqiy na masomo yake kuhusu Qur’an).
  • 4- Shekh Adnaan Hassaniy Ramishiy, utafiti wake ulihusu: (Usulu katika mtazamo wa Allaama Hilliy na athari yake katika vipimo vya maarifa ya dini).
  • 5- Dokta Jawaad Habib Albadraniy, utafiti wake ulihusu: (Qaswida za Sayyid Jafari Hilliy).
  • 6- Muqadam Abdulhassan Fayaadh, utafiti wake ulihusu: (Kalamu za Najafu katika misingi ya Hilla, Muhammad Ali Kamalu-dini na kitabu chake –Najafu Ashrafu katika robo karne toka 1908- kama mfano).
  • 7- Dokta Dhai’i Hasuum, utafiti wake ulihusu: (Mchango wa madrasa ya Hilla katika vitabu vya historia (500-800 hijiriyya)).
  • 8- Dokta Yahya Kadhim Maamuriy, utafiti wake ulihusu: (Msimamo wa wanazuoni wa Hilla katika vita ya Maghuliy nchini Iraq).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: