Katika kukumbuka tukio liumizalo la kufariki kishahidi kwa imamu Mussa bun Jafari (a.s), Atabatu Abbasiyya kama zifanyavyo Ataba zingine za Iraq imetangaza kipindi cha huzuni kufuatia kubadilishwa kwa bendera za maimamu watukufu Jawadain Kadhimai (a.s) kwa kukumbuka misiba na matatizo aliyo pata imamu Kadhim (a.s) kuanzia kufariki kishahidi kwa baba yake Swadiq hadi kufariki kwake (a.s).
Kuta za malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zimepambwa kwa vitambaa vyeusi na mabango yaliyo andikwa riwaya tukufu zinazo kumbusha tukio hili la kusikitisha, na zimepandishwa bendera nyeusi na kuwashwa taa nyekundu kama ishara ya kuomboleza msiba huu na kuwapa pole Ahlulbait (a.s).
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba kamili ya maombolezo haya, pamoja na kushiriki katika utoaji wa huduma kwa watu wanao kwenda kuwazuru maimamu wawili Kadhimain (a.s) katika mji mtukufu wa Kadhimiyya.