Chuo cha masomo ya kibinadamu chajadiliana na chuo cha Ilaam kuhu kufungua ushirikiano..

Sehemu ya mkutano wa viongozi wa chuo
Chuo cha masomo ya kibinadamu kimepokea ugeni mkubwa kutoka chuo cha Ilaam cha Iran ukiongozwa na dokta Muhammad Ali Akbari rais wa chuo hicho akifuatana na jopo la walimu wake, walipokewa na mkuu wa chuo dokta Swafaa Abduljabaar Ali Mussawiy, waka karibishwa katika ukumbi wa utawala na kujadiliana namna ya kufungua milango ya ushirikiano baina ya vyuo vyao.

Ugeni huo uliambatana na walimu wa chuo cha Waasit, ulitembelea maeneo ya chuo katika mji wa Najafu Ashrafu, na wakapewa waelezo ya kina na viongozi wa vitengo mbalimbali kuhusu vitendea kazi na ratiba ya masomo katika chuo hicho, walipewa maelezo pia kuhusu idara ya lugha inayo ongozwa na Mahmood Swabaar kua ndio wenye jukumu la kufundisha lugha ya kifarsi kwa wanafunzi wa chuo cha Firdausi.

Baada ya kumaliza matembezi yao, rais wa chuo cha Ilaam alisema kua: “Baada ya kukagua masomo yanayo fundishwa na chuo yametupa hamasa zaidi ya kuingia makubaliano ya kusaidiana kielimu na kitamaduni na chuo hiki cha masomo ya kibinadamu, kutokana na sifa nzuri iliyo nayo miongoni mwa vyuo vya Iraq, hali kadhalika tumekubaliana kuwapokea wanafunzi walio kubaliwa kujiunga na masomo ya juu katika chuo cha Ilaam kwa wanaotaka kusoma kozi za lugha ya kifarsi inayo fundishwa na idara ya lugha katika chuo cha masomo ya kibinadamu”.

Kumbuka kua chuo cha masomo ya kibinadamu kutokana na juhudi zake za kujenga ushirikiano na taasisi za kisekula za kimataifa, imesha ingia mikataba zaidi ya kumi ya ushirikiano na vyuo vya kiarabu na kimataifa na miongoni mwa vyuo hivyo ni vyuo vya nchini Iran.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: