Imamu Mussa Kadhim (a.s) aliishi muda mwingi wa uhai wake katika jela zenye giza, alikua anahamishwa jela moja hadi nyingine, alifungwa leja na Muhammad Mahadi Al-abbasiy kisha akamuachia, akafungwa tena na Haruna Rashidi Al-abbasiy katika mji wa Basra kwa Issa bun Jafari, kisha akamuhamishia katika jela ya Fadhlu bun Rabii katika mji wa Bagdad, kisha akapelekwa katika jela nyingine ya Fadhlu bun Yahya, na jela ya mwisho alilopelekwa imamu wetu katika mji wa Bagdad ni ile la (mal-uuni) Sindi bun Shaahik yenye adhabu kali na giza nene, ulikua haujulikani usiku wala mchana.
Imamu wetu mtakasifu (a.s) akiwa ugenini alidhulumiwa na wafalme wa zama zake, alipata maudhi na matatizo makubwa kutoka kwa mafasidi na waovu hoa, akiweme mal-uuni Mauhammad Mahadi aliye kusudia kumuua imamu (a.s) lakini Mwenyezi Mungu alimuangamiza kabla hajatekeleza azma yake, na baada yake mwanaye Haruna alimfunga imamu mara mbili.
Sindi bun Shaahiki iliwafanyia uadui mkubwa Ahlulbait (a.s) na ndiye aliye amrishwa na Haruna ampe sumu imamu (a.s), akampelekea imamu (a.s) punje kumi za tende zenye sum na akamuamrisha azile, imamu akala tende zile na akaanza kuugua, aliumwa siku tatu ndipo akafa kishahidi kutokana na sumu aliyo kula, alifia ndani ya jela yenye giza nene akiwa amefungwa kamba siku ya Ijumaa tarehe ishirini na tano mwezi wa Rajabu mwaka wa mia moja themanini na tatu hijiriyya.
Walichelewesha kumzika kwa ajili ya kumdhalilisha na kumdharau, walichukua mwili wake mtukufu wakauweka juu ya daraja la Raswaafah katika mji wa Bagdad, ukakaa siku tatu kama muili wa babu yake Mtume (s.a.w.w) na babu yake Hussein (a.s) kisha akazikwa (a.s) magharibi ya mji wa Bagdad katika makaburi yanayo julikana kama (makaburi ya makuraishi) kitongoji cha Karakh katika eneo la Kadhimiyya –Babu Tini- na ndio sehemu lilipo kaburi lake hadi leo.