Watumishi wa Alkafeel watoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa maimamu wawili Jawadain (a.s)..

Maoni katika picha
Kutokana na mapenzi yao kwa Ahlulbait (a.s) na kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kufariki kishahidi kwa imamu Mussa (a.s), watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kama kawaida yao kila mwaka, wamekuja kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa maimamu wawili Jawadain (a.s) wanao kuja katika mji mtukufu wa Kadhimiyya, wametoa huduma ya chakula, vinywaji, malazi na zinginezo.

Huduma zilizo tolewa ni hizi zifuatazo:

  • 1- Usafiri: makumi ya gari zinafanya kazi ya kubeba watu na kuwaleta katika eneo la haram tukufu.
  • 2- Kitengo cha mgahawa (mudhifu) cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinatoa chakula na kuandaa mikate ya haraka.
  • 3- Wana wapa mazuwaru na vikundi vya utoaji huduma (mawakib) matofali ya barafu kutoka katika kiwanda cha barafu cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 4- Wanawagawia mazuwaru makumi ya maelfu ya maji kutoka katika kiwanda cha maji cha Alkafeel.
  • 5- Kusambaza maji safi kwa makundi ya utoaji huduma (mawakib) kupitia magari maalim ya maji sasi.
  • 6- Wamefungua maeneo ya kugawa maji safi ya kunywa kwa kuweka madeli ya maji.
  • 7- Kushirikiana na watumishi wa Atabatu Kadhimiyya katika ratiba zao za kuimarisha usalama na utoaji wa huduma.

Kumbuka kua vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu hususan vinavyo husika na kutoa huduma, hushiriki katika kutekeleza ratiba za Ataba zingine katika vipindi vya ziara zao maalumu kutokana na uzoefu mkubwa walio nao katika utoaji wa huduma kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: