Katika siku kama ya leo kila mwaka watu wanaonyesha huzuni zao kwa msiba uliotokea, kundi kubwa la waumini wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wameenda katika malalo ya imamu Mussa Kadhim (a.s), wakiwa wamebeba jeneza la kuigiza katika siku ya kuuawa kwake kishahidi tarehe ishirini na tano mwezi wa Rajabu msiba ambao tupo katika maombolezi yake siku hizi.
Jeneza hilo lilirejesha kumbukumbu ya yaliyo jiri kwa imamu wete madhlumu, lilisindikizwa na umati mkubwa wa watu kuelekea katika uwanja wa haram tukufu ya Kadhimiyya.
Lilipokelewa kwa heshima kubwa kwa Qaswida na vilio kutoka kwa waombolezaji waliokua ndani ya haram tukufu, katika usindikizaji wa jeneza hilo alishiriki pia katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya tukufu na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi pamoja na watumishi wa Ataba hiyo tukufu, hali kadhalika kulikua na watu wengi muhimu kidini na kijamii pamoja na makundi ya waombolezaji (mawakib) waliyo kuja kwa miguu kuzuru (kutembelea) malalo ya maimamu watukufu (a.s), watu walijaa kila njia inayo elekea katika malalo matukufu kutoka ndani na nje ya Iraq, ratiba ya kusindikiza jeneza ilianza kwa Qaswida za kuomboleza na kuelezea msiba uumizao wa imamu Mussa Kadhim (a.s).