Kuna ibada na dua maalumu katika usiku wa Mab’ath miongoni mwake ni:
- 1-
- 2- Swala ya rakaa kumi na mbili iliyo pokewa kutoka kwa imamu Muhammad bun Ali Jawaad (a.s).
- 3- Ziara ya Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s).
- 4- Kusoma dua ya “Allahumma inni as-aluka bitajallil a’adhami fi hadhihi llailat mina shahril adhim..”.
Siku ya ishirini na saba Rajabu alipewa rasmi ujumbe wa uslamu mtukufu (s.a.w.w) miaka (13) kabla ya kuhama Maka na kwenda Madina, ulikua ni mwaka wa (610 m), Mwenyezi Mungu alimletea wahyi kupitia Jibril na kumjulisha rasmi kua yeye ni mtume wa umma huu na ndiye mtume wa mwisho..
Miongoni mwa ibada muhimu katika siku hii ni:
- 1-
- 2- Kufunga, atakae funga siku hii itakua kafara kwake kwa mwezi sitini.
- 3- Kukithirisha kumswalia mtume Muhammad na Aali zake watakatifu.
- 4- Ziara ya khatamul anbiyaa wa sayyidul mursalina Muhammad (s.a.w.w) na ziara ya Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s).
- 5- Kuswali rakaa thelathini, katika kila rakaa baada ya surat Fat-ha usemo surat Tauheed mara kumi.