Uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na washirika wake katika vita ya kukomboa mji wa Hadhwar katika oporesheni ya “Muhammad Rasulu Llah” iliyo anza asubuhi ya siku ya Juma Nne (27 Rajabu 1538 h) sawa na (25 April 2017 m) umetangaza kua kikosi cha Abbasi (a.s) na washirika wake wamepata mafanikio makubwa na wanasonga mbele katika vita ya kukomboa mji wa Hadhwar kufuatia kuzidiwa kwa magaidi ya Daesh kutokana na kipigo kikali wanacho pata.
Uongozi umesema kua: “Hadi sasa tumesha komboa zaidi ya kilometa 10, katika vita hii vimeshiriki vikosi mbalimbali vya Hashdi Sha’abi vikisaidiwa na vikosi vya anga vya jeshi la serikali ya Iraq, wakasisitiza kua hamasa ya wapiganaji ipo juu sana, wanatarajia kukomboa kitongoji hiki haraka iwezekanavyo na kupandisha bendera ya Iraq”.
Kumbuka kua oporesheni ya “Muhammad Rasulu Llah”, imeanza asubuhi ya siku ya Juma Nne katika pande tatu za mji huo kwa ushiriki wa vikosi mbalimbali vya Hashdi Sha’abi, kwa ajili ya kukomboa mji wa Hadhwar na vijiji vinavyo uzunguka vilivyo chini ya makaidi ya Daesh.