Picha mbele ya malalo tukufu ya imamu Ali (a.s), kundi la waumini wakihuisha kumbukumbu ya siku ya Mab’ath tukufu

Maoni katika picha
Yatupitia siku ya Mab’ath tukufu ambayo alipewa utume Muhammad (s.a.w.w), Jibril alimshukia na kumpa ujumbe wa utume, miongoni mwa ibada za siku hii tukufu ni ziara ya Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s) mbele ya malalo yake.

Makundi ya waumini wamekuja katika malalo ya Imamu Ali tukufu kuhuisha mnasaba wa siku hii, wamefurika ndani ya uwanja wa haram tukufu hadi nje watu kutoka semehu mbalimbali ndani na nje ya Iraq, vitengo vya Atabatu Alawiyya tukufu vimeongeza juhudi ya kutoa huduma kwa mazuwaru watukufu, wameandaa chakula kingi na maji pamoja na huduma za afya na za usafiri katika njia zote zinazo elekea katika malalo ya Amirulmu-uminina (a.s).

Mazuwaru wamewapongeza waislamu wote na Maraajii dini watukufu pamoja na raia wa Iraq kwa mnasaba huu na wamemuomba Mwenyezi Mungu awape ushindi wa haraka wapiganaji wa Hashdi Sha’abi na jeshi la serikali dhidi ya magaidi ya Daesh na wakomboe aridhi yote iliyo tekwa na magaidi hao.

Kumbuka kua tarehe ishirini na saba ya mwezi wa Rajabu waislamu huadhimisha siku ya Mab’ath; siku aliyo pewa utume Muhammad (s.a.w.w) miaka (13) kabla ya kuhama Maka na kwenda Madina mwaka wa (610 m) kwa njia ya wahyi kupitia malaika Jibril (a.s) aliye kuja na kumuambia kua yeye ni mtume wa umma huu na mwisho wa mitume.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: