Wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) wamekomboa vijiji vitatu na wanadhibiti barabara muhimu pia wamekutana na wapiganaji wengine

Maoni katika picha
Wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) wamekamilisha jukumu lao la kwanza katika kukomboa mji wa Hadhwar kusini mwa Mosul katika opreshen ya (Muhammad Rasulu Llah) iliyo anza asubuhi ya siku ya Juma Nne (17 Rajabu 1438 h) sawa na (25 April 2017 m), majemedari wa kikosi cha Abbasi (a.s) kama kawaida yao wamepigana kwa ushujaa na ujasiri mkubwa, wamewapa hasara kubwa magaidi ya Daesh, wamekomboa zaidi ya kilometa kumi na vijiji vitatu; kijiji cha Alwanin, Dabisah na Khanifas, na wamekutana na wapiganaji wengine wa Hashdi Sha’abi, vilevile wamedhibiti barabara muhimu inayo onganisha mji wa Hadhwar na Qirwaan iliyo kua inatumiwa na magaidi wa Daesh.

Kwa upande mwingine wahandisi wameanza kufungua ngome za udongo zilizo wekwa na magaidi ya Daesh pamoja na kutegua mapomu ya aridhini yaliyo tegwa majiani na magaidi hao ili kuhakikisha usalama wa raia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: