Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu aelekeza ufunguzi wa kituo cha kutengeneza viungo bandia katika hospitali ya Alkafeel baada ya kuchukua jukumu la kuwapa viungo bandia majeruhi wa Hashdi Sha’abi..

Maoni katika picha
Baada ya kufanikiwa kufunga miguu sita bandia awamu ya kwanza, wataalamu wa hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanikiwa kufunga miguu bandia (11) bure kwa wapiganaji wa Hashdi Sha’abi, walio poteza miguu yao katika vita ya kukomboa aridhi tukufu ya Iraq, na wameweza kuingiza utaratibu huu rasmi katika hospitali kutokana na uzoefu wao katika swala hilo.

Kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) katika matembezi yake na kukagua maendeleo ya ufungaji wa miguu bandia yenye teknolojia ya kisasa inayo muwezesha majeruhi kutembea, ameuambia uongozi wa hospitali kuanzisha kituo rasmi cha kutengeneza na kufunga viugo hivyo, na uongozi wa hospitali umeonyesha utayali wake wa kufungua kituo hicho.

Kiongozi mkuu wa hospitali dokta Haidari Bahadeli amesema kua: “Kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmad Swafi amepongeza kazi ya kuwafunga miguu bandia wapiganaji wa Hashdi Sha’abi walio poteza mikuu yao katokana na majeraha waliyo pata katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh, wapiganaji hao ni kutoka katika mikoa tofauti ya Iraq, walipata matibabu bure katika hospitali ya Alkafeel kwa wakati tofauti”.

Akaongeza kusema kua: “Viungo bandia vinavyo tumika ni vya kielektonik vilivyo tengenezwa kisasa zaidi, vitawasaidia kuendesha maisha yao katika hali ya kawaida, vimetengenezwa kwa program ya (MMS) hufungwa kwa mgonjwa ndani ya saa mbili, na baada ya hapo mgonjwa anaweza kutembea moja kwa moja, njia hii inatofautiana na njia ya zamani iliyo kua inachukua hadi siku tatu”.

Kumbuka kua hostitali ya rufaa Alkafeel ni sawa na taasisi zingine za Atabatu Abbasiyya tukufu, toka ilipo tolewa fatwa tukufu ya kuilinda Iraq na maeneo yake matukufu, wamechukua jukumu la kusaidia majeruhi wa wapiganaji ili kupunguza matatizo na maumivu yao, kutokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu yanayo sisitiza jambo hilo, pia ni jukumu lao kuwatibu majeruhi na kuwapa viungo bandia wapiganaji walio poteza viungo vyao vitani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: