Uhudhuriaji wa makatibu wakuu: Kuanza kongamano la Ataba na Mazaru tukufu zilizopo katika ulimwengu wa kiislamu..

Maoni katika picha
Siku ya Juma Tano (28 Rajabu 1438 h) sawa na (26 April 2017 m) katika Atabatu Husseiniyya tukufu, limeanza kongamano la pili la Ataba na Mazaru tukufu zilizopo katika ulimwengu wa kiislamu, linalo hudhuriwa na Atabatu Alawiyya, Kadhimiyya, Radhawiyya, Askariyya, Abbasiyya, Zainabiyya, pamoja na baadhi ya Mazaru tukufu, chini ya kauli mbiu isemayo: (Haki za mazuwaru ni amana katika shingo zetu), kongamano hili litadumu siku tatu, linajadili mfumo utakao fuatwa kwa pamoja na Ataba zote, utakao pelekea kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa malalo na Ataba tukufu.

Kongamano hili limehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya tukufu na makatibu wakuu wa Ataba na Mazaru tukufu, lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya tukufu Shekh Abdulmahad Karbalaiy (d.i) akaongea, miongoni mwa aliyosema ni: “Hakuna shaka kua mambo yanayo ziunganisha Ataba tukufu kwanza: tunaungana katika lengo moja, pili: umuhimu wa kudhihirisha hilo, tatu: tunafanya kazi ya aina moja katika kutekeleza majukumu ya Ataba zetu, utaratibu wa ulimwengu umeumbwa kwa kutegemeana, baadhi inategemea baadhi nyingine hakuna kitu ambacho kimekamilika na hakitegemei kitu kingine, hivyo hivyo ili kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi ni lazima tusaidiane, kwa kushirikiana sote tutaimarika, tutakapo kubaliana vupengele vya kushirikiana na kuweka utaratibu wa utekelezaji, lazima sote jambo hili tulipe kipawa mbele zaidi, lazima tutekeleze makubaliano hayo kwa bidii zaidi, kufanya kazi kwa kushirikiana kutatuwezesha kunufaika haraka, tujiepushe na kila jambo linalo tutenganisha, tuhakikishe sote kwa pamoja tunashikamana na mambo yanayo tuunganisha”.

Kisha akazungumza rais wa wakfu wa shia Sayyid Alaa Mussawiy, akasema kua: “Tujikite katika kuchagua mambo mazuri na tuwe makini katika mambo ambayo tunatakiwa kushirikiana, tunatoka nchi tofauti, jamii tofauti pengine na mazingira tofauti, lakini ni ukweli kua zinapo ungana nchi mbili au kundi la watu fulani katika lengo moja na wakashirikiana kutekeleza lengo lao, mara nyingi ushirikiano wao huwanufaisha na huwapa faida nyingi, itakua vipi kwa sisi ambao tupo ndani ya chungu kimoja tuna fikra moja ya kumtawalisha Mwenyezi Mungu mtukufu na mitume wake pamoja na waja wake wema, imani yetu imejengwa kutokana na asili moja na lengo moja, bila shaka ushirikiano huu wa Ataba tukufu na malalo ya mawalii pamoja na sehemu tukufu za ibada utakua na faida kubwa sana, hususan tutakapo kua makini kuanzia mwanzo katika kubaini malengo na maeneo ya kuungana”.

Kulikua na michango mingi ya mazungumzo iliyo tolewa na makatibu wakuu wa Ataba tukufu za Kadhimiyya, Radhawiyya, Askariyya pamoja na makatibu wakuu wa Mazaru tukufu, wote walisisitiza umuhimu wa kushirikiana baina ya Ataba tukufu na kuunganisha juhudi zao katika utoaji wa huduma kwa watu wanao kuja kufanya ziara na umuhimu wa kubadilishana uzoefu pamoja na kua wanatoka nchi tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: