Wakaongeza kusema kua: “Tafiti zilizo wasilishwa katika shindano hilo zilikua zaidi ya hamsini, zote zilikidhi vigezo na kuingizwa katika shindano, kazi ya kuzishindanisha ilichukua majuma kadhaa, na mwisho tafiti za kinadada wanne zikaibuka na ushindi ambao ni:
- 1- Rana Khawiladi/ kutoka Najafu Ashrafu, utafiti wake unasema: (Mbora wa wanawake wa zama zake Sukaina bint Hussein (a.s) baina ya mateka na uzushi wa kihistoria)
- 2- Dokta Aliya Rasan Muyassar/ utafiti wake unasema: (Mtazamo wa matatizo na matatizo ya mtazamo.. kusoma katika Makala za bibi Zainabu (a.s) –Sikuona ispokua uzuri-).
- 3- Dokta Basaam Ali Hussein Amiriy na Sam Mahadi Ahmad/ utafiti wao unasema: (Umuhimu wa vyombo vya habari katika kulingania uislamu).
- 4- Radhiyah Sadati Sajadi/ kutoka Iran, utafiti wake unasema: (Hotuba ni njia ya mtazamo wa akhera).