Chini ya usimamizi wa Maahadi Alkafeel ya kulea vipaji: Kitivo cha sayansi ya kompyuta katika chuo kikuu cha Karbala chafanya maonyesho ya kitalamu na program za kompyuta..

Maoni katika picha
Kitivo cha sayansi ya kompyta katika chuo kikuu cha Karbala asumuhi ya Juma Tano (28 Rajabu 1438 h) sawa na (26 April 2017 m) wamefanya maonyesho ya kitalamu yaliyo husisha wanafunzi wa chuo kuhusu ujuzi wa kompyuta na program zake chini ya usimamizi na ulezi wa Maahadi Alkafeel ya kulea vipaji, ambayo ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, maonyesho haya yanahusisha vitu vingi vilivyo fanywa na wanafunzi wa sayansi ya kompyuta hatua ya nne, Maahadi ya Alkafeel kwa upande wake ilionyesha mafanikio iliyo pata katika kubuni na kuanzisha program za kompyuta pamoja na ufunguzi ya toghuti.

Jambo hili linafanyika kutokana na mpango wa Ataba tukufu wa kufungua mlango wa kushirikiana na taasisi za kisekula kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali, kiongozi wa kitengo cha usanifu wa Maahadi Alkafeel Ustadh Alaa Abdulhamid aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Chini ya usimamizi wa Maahadi Alkafeel, wanafunzi wa kitivo (mchepuo) wa sayansi ya kompyuta katika chuo kikuu cha Karbala wameweza kuonyesha ujuzi mbalimbali wa fani za kompyuta walizo hitimu, zikiwepo program tofauti katika sayansi ya kompyuta, kama mnavyo fahamu; Maahadi Alkafeel iliajiri idadi fulani ya wahitimu wa chuo hiki miaka ya nyuma, na sasa inaendelea kua mlezi wa kitivo hiki kwa ajili ya kunufaika na wahitimu katika Ataba tukufu au katika taifa kwa ujumla, na huwapatia semina mbalimbali za kuongeza uwezo katika fani wanazo somea, leo hii tumeandaa maonyesho haya baada ya kuandaa wanafunzi (49) wa fani tofauti, pia Maahadi imechukua jukumu la kuwapa zawadi wanafunzi watakao fanya vizuri, pamoja na kuwapa ofa ya semina za kujenga uwezo (IQ) pia watapewa kozi ya Exsel, Photoshop na zinginezo”.

Naye rais wa chuo cha Karbala Ustadh Munir Hamid Saidiy alisema kua: “Kwa hakika tunafuraha kubwa sana kuwa na ushirikiano mkubwa kiasi hiki na Maahadi Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kitivo cha sayansi cha chuo kikuu cha Karbala, ushirikiano huu ulipelekea kuajiriwa kwa wahitimu wa masomo ya sayansi ya kompyuta na Maahadi hii, pamoja na kudumisha ushirikiano katika maswala ya kisekula na kitalamu kuhusu kompyuta, tunaishukuru sana Maahadi Alkafeel kwa kuwapa zawadi wahitimu wa mwaka huu, pamoja na kuchangia mishahara ya watalamu wa pande zote mbili, tunajitahidi daima kuenzi ushirikiano wetu na kuhakikisha unaboreka zaidi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: