Katibu mkuu wa Mazaru za Iraq atembelea korido za maonyesho ya vitabu ya kimataifa huko Karbala na asifu ufanisi wa mpangilio wake..

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Mazaru za kishia nchini Iraq Shekh Sataar Jizani amesifu mpangilio mzuri wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Karbala pamoja na juhudi zinazo fanywa na wasimamizi wa maonyesho hayo, ambao wamefanikiwa kuyafanya kua katika muonekano bora zaidi kutokana na kuzipanga vizuri taasisi za uchapaji na usambazaji zinazo shiriki katika maonyesho haya.

Aliyasema hayo alipo tembelea maonyesho yanayo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Ili tusome pamoja) ambayo ni sehemu ya shughuli za kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu ambalo litaanza mwezi tatu Shabani, Shekh Jizani alipokelewa na mkuu wa kitengo cha maonyesho Ustadh Muyassar Hakim na alimpa maelezo kwa ufupi kuhusu maonyesho na taasisi zinazo shiriki, Hakim alisikiliza kwa makini maelezo aliyo pewa na Shekh Jizani.

Uongongozi mkuu wa Mazaru umeshiriki katika maonyesho haya kupitia kitengo cha elimu, utamaduni na habari kutoka katika Mazaru tofauti, wameonyesho machapisho yao na vitabu vya kidini na kitamaduni bamoja na folda za utambulisho zikiwemo na kauli za maimamu watakatifu (a.s).

Kumbuka kua maonyesho ya vitabu ya kimataifa ya Karbala ni moja ya shughuli muhimu za kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa linalo andaliwa na kugharamiwa kwa ukamilifu na Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) toka kuanzishwa kwake kabla ya miaka zaidi ya kumi na moja iliyo pita, ambalo hufanyika kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) imamu Abuu Abdillah Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: