Kamati inayo simamia kongamano la msimu wa elimu la kimataifa awamu ya tatu litakalo anza kesho Ijumaa (28 April 2017 m) katika mji mkuu wa Malesia Kwalalumpa yakutana na ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu uliokwenda kushiriki na ambao ni moja ya walezi wa kongamano hilo.
Kikao hicho kilihudhuriwa na dokta Ashrafu Muhammad Zidani kiongozi mkuu wa kongamano, dokra Yusufu Swedi mjumbe wa uongozi mkuu na Ustadhi Ibrahim Ghanim mjumbe wa kamati ya uongozi wa kongamano la kimataifa la msimu wa kielimu awamu ya tatu, walijadiliana kuhusu kushiriki kwa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kongamano la (2017 m) ambalo litafanyika (28-29 April), katika ukumbi wa hoteli ya Milya katikati ya mji mkuu Kwalalumpa.
Mjumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Ali Swafar aliwasilisha salamu maalumu za Ataba kwa wajume na wasimamizi wote wa kongamano hili, akawaelezea mafanikio muhimu yaliyo patikana katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa muda wa miaka zaidi ya kumi na tano, akataja baadhi ya mambo yanayo fanywa na kitengo cha habari na utamaduni, kama vile kuandaa makongamano ya kimataifa, machapisho mbalimbali na kushajihisha kufanywa tafiti za kielimu.
Pia Swafar ametoa wito kwa kamati inayo simamia kongamano hili kuzuru Atabatu Abbasiyya na kuangalia maendeleo yake katika miradi mbalimbali, na urithi mkubwa ilio nao wa turathi na nakala kale, akawatakia mafanikio mema na kuwaomba waendelee kubuni makongamano kama haya kwa ajili ya kuleta faida zaidi kwa kunufaika na elimu tofauti na wanachuoni mbalimbali.
Kamati inayo simamia kongamao ilifurahishwa sana na mafanikio yaliyo fikiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu waliyo elezewa, wakavutiwa sana kufungua ushirikiano na kusaidiana baina yao.