Muitikio unaongezeka katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa mjini Karbala, wadau wakiri kua ni moja ya mafanikio..

Maoni katika picha
Maonyesho ya vitabu awamu ya kumi na tatu katika siku ya nne yanayo fanyika katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), yanapata muitikio mkubwa wa watu wa rika zote kutoka ndani na nje ya Karbala bali hata kutoka nchi za nje, yamechangamka sana baada ya alasiri ya siku ya Alkhamisi, mazuwaru wengi wametumia muda huo kutembelea maonyesho na kuangalia vitu vilivyopo katika maonyesho haya.

Upatikanaji wa vitu mbalimbali katika maonyesho haya ni sababu kubwa ya kuwepo kwa mwitikio huu, maonyesho haya ni sawa na kapu lililo jaa aina zote za fikra za kisekula, kididi, kitamaduni, pamoja na tamaduni za watoto na wanawake na vinginevyo, sababu nyingine ya mwitikio huu kwa mujibu wa wadau ni mpangilio mzuri uliopo, unao muwezesha mtu kutembea kwa urahisi na kuangalia kila kilichopo katika maonyesho, pia mwitikio huu unamaanisha kua maonyesho yamefanikiwa kwa kiwango cha kimataifa, na yanashinda maonyesho mengi ambayo hufanyika ndani au nje ya Iraq.

Kumbuka kua eneo yanapo fanyika maonyesho haya lina ukubwa wa (3000m2) na zinashiriki zaidi ya taasisi za usambazaji (165), jumla ya nchi zinazo shiriki ni (9), za kiarabu na zisizokua za kiarabu, ambazo ni: Misri, Lebanon, Iran, Sirya, Jodan, India, Kuwait, Saud Arabia, Algeria ukiongeza na mwenyeji wao Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: