Hivi punde.. Osifi ya Ayatullah Sayyid Sistani (d.dh) yatangaza kua kesho ni mwezi mosi Shabani..

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Sistani (d.dh) imetangaza kua Ijumaa ya kesho (28 April 2017) ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Shabani (1438 h).

Ofisi ya Marjaa dini mkuu Ayatullah Sayyid Sistani (d.dh) ilikua inategemea kuandama kwa mwezi jioni ya leo siku ya Alkhamisi (27 April) kutokana na mwenendo wa nyakati za mwandamo.

Mtandao wa Alkafeel wa kimataifa na watumishi wake wote unamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu kwa baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s), aujalie mwezi huu na mwezi mingine yote kua yenye baraka kwa nchi ya Iraq na raia wake pamoja na nchi zote za kiislamu hakika yeye ni msikivu na mjibuji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: