Haya ndio yaliyofanikishwa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika vita ya kukomboa mji wa Hadhwar..

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimetangaza mafanikio kiliyopata katika vita ya kukomboa mji wa Hadhwar katika oporeshen ya (Muhammad Rasulu Llah), walikamilisha utekelezaji wa jukumu walilo pewa kwa muda mfupi sana; wa saa tano. Ndani ya muda huo walifanikisha mambo yafuatayo:

  • A- Kukomboa kilometa (106).
  • B- Kukomboa vijiji vinne (Albu-ulum, Majhula, Dubais na Khanifas).
  • C- Kuua magaidi na kuteka madaesh wawili.
  • D- Kupokea familia za wakimbizi (105) na kusaidia kuwatoa katika maeneo yenye vita.

Katika vita hii vikosi vifuatavyo vilishiriki:-

  • 1- Kikosi cha deraya kimeshiriki rasmi kwa mara ya kwanza pamoja na Hashdi Sha’abi.
  • 2- Vikosi vya watembea kwa miguu (Alkafeel na Alqami).
  • 3- Kikosi cha makomandoo

Pamoja na kikosi cha wahandisi, vifaru, ndege zisizo kua na rubani na ulinzi wa kielektronik wakiwemo na wasimamizi wa oporeshen.

Wasimamizi walikua ni:

  • A- Kamati ya viongozi wa Hashdi Sha’abi.
  • B- Viongozi wakuu ya oporeshen ya (Tunakuja ewe Nainawa) na viongozi wa oporeshen ya pamoja.
  • C- Wizara ya ulinzi iliwajibika kutoa siraha.
  • D- Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutoa msaada wa kiufundi na mishahara ya wapiganaji kwa asilimia kubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: