Kuingia kwa mwezi wa Shabani na kuzaliwa kwa nuru za Alawiyya: Atabatu Abbasiyya tukufu yapendezesha muonekano wake..

Maoni katika picha
Mwezi wa Shabani una utukufu wake, siku zake zina matukio muhimu katika nyoyo za waumini, kuna kumbukumbu ya kuzaliwa maimamu watakasifu, Imamu Hussein bun Ali na ndugu yake Abbasi na mwanae imamu Ali bun Hussein (a.s) pia kuna kumbukumbu ya kuzaliwa kwa imamu Hujjah bun Hassan Almahadi (a.f) tarehe kumi na tano ya mwezi huu.

Mwezi wa Shabani ndio huu umeshaingia kwa furaha na mapenzi, mwezi wa kupongezana kwa shangwe tofauti na miezi mingine, mwezi huu umebeba furaha za Ahlulbait (a.s), wapenzi wa mtume Muhammad na watu wa nyumani kwake huwa na furaha kutokana na matukio yaliyopo ndani ya mwezi huu, hivyo haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imepambwa ndani na nje na katika korido zake kwa kuweka maua ya aina mbalimbali yenye rangi nzuri za kupendeza machoni, hali kadhalika imepambwa hadi minara yake na ukuta wa haram tukufu umewekwa taa za rangi zinazo ashiria furaha kutokana na minasaba ya mazazi iliyo mbele yetu, mapambo haya yamefanywa kwa kufuata ramani ya upambaji iliyo andaliwa rasmi kutokana na minasaba hii.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalumu ya kuhuisha kumbukumbu ya minasaba iliyopo ndani ya mwezi huu mtukufu, ndani ya ratiba hiyo kuna mambo mengi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: