Kamati ya habari ya kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa yazindua vitabu viwili..

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu ambalo litaanza jiono ya kesho Juma Pili chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein (a.s) ni kisima kirefu na chemchem endelevu) kwa usimamizi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) imezindua vitabu viwili, kimoja kinaelezea yaliyo jiri katika kongamano lililopita na kingine kinaelezea mchango wa Marjaiyya dini mkuu kwa wakimbizi toka kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kamati hiyo na naibu rais wa kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Aqeel Yasiriy, aliongeza kusema kua: “Miongoni mwa malengo iliyo jiwekea kamati ya habari ni kutoa kitabu kinacho elezea yaliyo jiri katika kongamano lililo pita kwa ufupi, kuanzia hafla ya ufunguzi hadi hafla ya kufunga ambapo huchukua siku tano kwa jina la (Yaliyo jiri katika kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na mbili)”.

Akaendelea kusema kua: “Toleo la pili tulilo liweka mikononi mwa wageni wa kongamano, limejikita katika kuelezea mchango uliotolewa na watu wa heri, na kimepewa jina la (Miongoni mwa juhudi za kihistoria na kibinadamu za Marjiiyya dini mkuu katika kuwasaidia wakimbizi toka kuanza kupatikana kwao, namna gani wamesaidiwa na wanaendelea kusaidiwa hadi sasa. Vimeandikwa kwa lugha mili, kiarabu na kiengereza”,

Kumbuka kua kamati ya habari imebeba majukumu kadhaa, miongoni mwa majukumu yake ni; kuchapisha vitabu, kutoa folda, broshua na majarida mbalimbali, pamoja na kuendesha shughuli za matangazo ya kongamano na kuwasiliana na vyombo vya habari pamoja na kuwawekea mazingira rafiki ya kutekeleza majukumu yao, kuanzia wapiga picha hadi wale wanao wahoji wageni wa kongamano, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kongamano linatangazwa kila siku katika vyombo vya habari vya Ataba mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) na kuufikisha ujumbe wa kongamano mbali zaidi kwa namna inavyo wezekana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: