Pamoja na kukumbuka kuzaliwa kwa imamu Hussein (a.s) nyoyo za wapenzi wake hukumbuka wito wa (waa Husseinaahu) unao patikana katika riwaya zinazo endelea kutajwa na wafusi wake milele..
Siku ya tatu ya mwezi wa Shabani mwaka wa tatu hijiriyya iliangaza nuru ya kuzaliwa kwa imamu Hussein bun Ali bun Abuutwalib (a.s), siku ya kuzaliwa kwake ilichanganyika furaha kwa kuzaliwa kwake na huzuni ya kuuawa kwake kishahidi, alipo kuja Jibril kwa Mtume (s.a.w.w) kumpa habari ya kuzaliwa kwake na hapo hapo akampa taarifa ya kuuawa kwake, imamu Hussein (a.s) alizaliwa katika mji wa Madina ndani ya nyuma ya wazazi wake iliyo kua jirani na nyumba ya Mtume (s.a.w.w), katikati ya msikiti wa mtume ambayo ni miongoni mwa sehemu tukufu zaidi katika aridhi, amelelewa chini ya usimamizi wa babu yake mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), akajifunza tabia njema kutoka kwa mtume na ushujaa, alikua anafanana sana na babu yake mtume wa Mwenyezi Mungu kama alivyo fanana na kaka yake imamu Hassan (a.s). Mtume (s.a.w.w) aliswali rakaa mbili kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuzaliwa kwake na akamfanyia hakika siku ya saba ya umri wake.
Imepokewa kutoka kwa Shekh Tusi (r.a) na wengineo kwa mapokezi yenye nguvu kutoka kwa imamu Ridha (a.s) anasema: (…Asmaa alisema: Fatuma alipo mzaa Hussein (a.s) alikuja mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: niletee mwanangu ewe Asmaa, nikampelekea akiwa kwenye kitambaa cheupe, akamfanyia kama alivyo fanya kwa Hassan (a.s) kisha akasema: akalia mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) halafu akasema: hakika utauawa, Mwenyezi Mungu amlaani atakaye kuua, (akaniambia) usimuambie Fatuma jambo hili, Asmaa akasema: ilipo fika siku ya saba, Mtume (s.a.w.w) alikuja akasema, niletee mwanangu, nikampelekea, akamfanyia hakika kwa kuchinja mbuzi na akamnyoa nywele kisha akatoa sadaka ya hela kwa uzito wa nywele, halafu akamlea na kusema: Ewe Abaa Abdillah kipenzi! ole wake atakaye kuua, kisha akalia, akasema (Asmaa), kwa haki ya baba, wewe na mama yangu ulifanya hivi siku ya kwanza na leo pia, unamaana gani? (mtume) Akasema: Namlilia mwanangu huyu atauliwa na watu waofu walio kufuru katika bani Umayya, Mwenyezi Mungu awalaani na hawatapata shufaa yangu siku ya kiyama, atauliwa na mtu anaye jiidata mtu wa dini huku anamkufuru Mwenyezi Mungu mtukufu, kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu ninakuomba kuhusu Hassan na Hussein (a.s) kama alivyo kuomba Ibrahim kuhusu familia yake, Ewe Mwenyezi Mungu wapende na umpende atakae wapenda na umlaani atakae wachukia, laana ya kujaa mbungu na aridhi.
Shekh Kuleiniy katika Usulu Kafi amepokea riwaya kutoka kwa imamu Swadiq (a.s) anasema: (Imamu Hussein hakunyonya kwa bibi Fatuma (a.s) wala kwa mama yeyote, mtume (s.a.w.w) alikua anampa kidole ananyonya hadi anashiba kiasi ya siku mbili hadi tatu, mwili wa Hussein (a.s) umejengeka kutokana na mwili wa mtume (s.a.w.w), na hakuna aliye zaliwa kwa (ujauzito) wa miezi sita ispokua Nabii Issa bun Maryam na Hussein bun Ali (a.s).