Hivi punde: Kuanza kwa kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu..

Maoni katika picha
Kabla ya muda mfupi alasiri ya leo Juma Pili (3 Shabani 1438 h) sawa na (30 April m) limeanza kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu, linalo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein (a.s) ni kisima kirefu na chemchem endelevu) chini ya usimamizi wa Ataba mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) tukufu.

Ratiba ya kwanza ya kongamano hili ni hafla ya ufunguzi inayo fanyika muda huu katika haram tukufu ya Abuu Abdillahi Hussein (a.s) ikihudhuriwa na idadi kubwa ya wageni maalum wa kidini, kitamaduni, kijamii na kundi kubwa la waumini.

Hafla hii ina mambo mengi, muhimu katika hayo ni; ujumbe wa Ataba mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) utakao wakilishwa na muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi, kisha ujumbe wa wakfu shia, halafu utafuata ujumbe wa bara la Asia, Afrika, Ulaya na bara la Amerika, pamoja na qaswida za kimashairi kuhusu utukufu wa Ahlulbait (a.s).

Tutakujuzeni kwa urefu zaidi kongamano litakapo isha inshallah.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: