Kiongozi wa kikundi cha Muridi aonyesha utayari wake wa kusaidiana katika wema na ucha Mungu pamoja na kila anayetaka kufanikisha umoja katika Umma wa kiislamu..

Shekh Shuaibu Kibiy
“Shekh wa kikundi cha Mridi katika nchi ya Senegal na Afrika kwa ujumla Shekh Sayyid Mukhtaar Jakir ameonyesha utayali wake wa kushirikiana na Ataba tukufu za Iraq au mtu mwingine yeyote kwa ajili ya kujenga umoja wa umma wa mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuifanyia kazi aya isemayo: (Saidianeni katika wema na ucha Mungu wala msisaidiane katika makosa na uadui), kutokana na ukubwa wa umri wake na wingi wa majukumu aliyo nayo hakuweza kuhudhuria yeye mwenyewe lakini yuko pamoja na nyie kwa moyo wake”.

Hayo yalisemwa na Shekh Shuaibu Kibiy kwa niaba yake ambaye aliwakilisha bara la Afrika katika ufunguzi wa kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu, lililo anza alasiri ya Jumapili (3 Shabani 1438h) sawa na (30 April 2017 m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein (a.s) ni kisima kirefu na chemchem endelevu).

Akaongeza kusema kua: “Katika Rabiu Shahada kutokana na mnasaba wa kuzaliwa kwa kielelezo cha shahada, kujitolea na ushujaa na kuzaliwa kwa ndugu yake Abulfadhil Abbasi (s.a) tunatoa salamu za pongezi kwa bara lote la Afrika ambalo linaonyesha mapenzi kwa Mtume (s.a.w.w) na Ahlubait wake watukufu (a.s)”.

Akaongeza kua: “Vilevile nazipeleka salamu kwa Ataba tukufu kutoka kwa Shekh Sayyid Mukhtaar Jakir Khalifa wa twarika ya Muridi kwa ndugu zake katika dini na wafuasi wote wa Ahlulbait (a.s) hususan ndugu zake wairaq, na kwa namna ya pekee kabisa wale wanao simamia kongamano hili, Shekhe anashukuru sana kwa kumpa mwaliko huu mtukufu, huwachukulia wafuasi wa Ahlulbait kua ni ndugu zake na wapenzi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w), sisi sote tunaonganishwa na kumpenda Mwenyezi Mungu pamoja na kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w)”.

Akamaliza kwa kusema: “Sisi tunaamini umuhimu wa umaoja wa waislamu na dharura ya kuongea kwa maelewano, daima tunajenga undugu baina ya wafuasi wa Sufi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) pamoja na waislamu wote, mwisho Shekh anakuombeeni taufiq na mafanikio mema”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: