Mji wa Sayyid Auswiyaa (a.s) wawa mwenyeji wa kikao cha kutambuana wageni wa kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu..

Maoni katika picha
Jambo la pekee katika kongamano la Rabiu Shahada awamu ya kumi na tatu ni kuhudhuriwa na watu kutoka katika mataifa mbalimbali na wa tabaka tofauti, kwa ajili ya kutambuana wageni wetu watukufu, kamati ya maandalizi kama kawaida yake katika kila mwaka iliandaa kikao maalumu cha kutambuana katika siku ya kwanza ya kongamano hili linalo simamiwa na Ataba mbili tukufu (Husseeiniyya na Abbasiyya) chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein (a.s) ni kisima kirefu na chemchem endelevu) kikao hicho kilifanyika jioni ya jana Juma Pili (3 Shabani 1438 h) sawa na (30 April 2017 m).

Kikao kilifanyika katika mji wa Sayyid Auswiyaa (a.s) na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu Shekh Abdulmahad Karbalai (d.i) pamoja na makatibu wakuu wa Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano wakiwemo massayyid na mashekh watukufu pamoja na wasomi wa kisekula na waandishi wa habari.

Baada ya kufunguliwa kikao kwa Qur’an tukufu rais wa kamati ya maandalizi ya kongamano alisimama na kutoa ukaribisho kwa wageni, alitoa shukrani nyingi kwa kila aliye itikia wito huu na kuhudhuria katika mji wa Karbala kwa ajili ya kushiriki kongamano hili.

Baada ya hapo iliimbwa Qaswida ya kimashairi na kikao kilihitimishwa kwa kuonyesha filamu ya mkono wa kheri (Yadul Khauri), iliyo andaliwa na idara ya Alkafeel iliyo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, filamu hiyo inaelezea fatwa tukufu ya Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu muheshimiwa Sayyid Ali Sistaniy (d.dh) na nafasi yake katika kuitoa nchi kwenye shimo la moto baada ya kushambuliwa na maadui wa uislamu na ubinadamu, na namna fatwa hiyo ilivyo pokelewa na wananchi walio onyesha ubinadamu wa hali ya juu kabisa kwa kuwapokea na kuwasaidia wakimbizi wa dini na tabaka tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: