Sayyid Swafi: Daima tunapambana kuhakikisha tunaleta utulivu na amani katika nchi yetu, tunaendesha vita kali dhudi ya kikundi kilicho potea..

Sayyid Swafi
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) amewaambia wageni wa kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu, alio kutana nao katika kikao cha mapumziko kinacho tenganisha baina ya vikao vya asubuhi na vya jioni kua: “Hakika tunapambana daima kuleta amani na utulivu katika nchi yetu, wairaq wanaendesha vita kali –wavulana kwa wasichana wazee kwa vijana- wote wamesimama pamoja dhidi ya kundi lililo potea”.

Akaongeza kua: “Tunafuraha kubwa kutembelewa na ugeni huu mtukufu katika siku hizi za Rabiu Shahada, kongamano hili linafaida nyingi sana, miongoni mwa faida zake ni kujuana na kujenga undugu baina yetu, kila mwaka hutujia ndugu watukufu wenye nafasi muhimu katika nchi zao, na wao hua mabalozi wazuri wa kusambaza ujumbe wa kongamano letu”.

Akabainisha kua: “Baadhi ya ndugu wanafanya kazi katika magazeti na wengine ni waandishi, sisi tuna haja kubwa ya kufikisha ujumbe kwa walimwengu, leo hii muandishi anajukumu la kusoma na kuandika kwa makini ili amfikishie msomaji wake kitu kizuri na cha uhakika, alhamdu lilahi nchi ipo salama kama mlivyoona, na sisi tunapambana daima kuhakikisha amani na usalama vinapatikana, tunaendesha vita kali dhidi ya kundi lililo potea”.

Akabainisha kua: “Wavulana kwa wasichana, wazee kwa vijana wote wamesimama pamoja kupambana katika vita hii, ambayo tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu ajalie vimalizike mapema iwezekanavyo, huenda kongamano letu la mwaka kesho likafanyika katika kazingira bora zaidi kuliko yalivyo leo inshaalaah”.

Akaongeza kusema kua: “Sisi tunafanya kazi na kila mtu kama ndugu, kwa hakika nyie ni ndugu zetu na sisi ni wageni kwenu, tuna muomba Mwenyezi Mungu mtukufu atukusanye pamoja na nyie katika mapenzi na amani, ujumbe wetu kwa wote ni kueneza mapenzi haya tunayo yaingiza katika vifua vyenu, tunatarajia tuone matunda yake katika vitendo hususan sisi tunao ishi chini ya bendera ya maimamu watukufu ambao ndio kielelezo cha ubinadamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: