Kamati ya maandalizi imetenga ratiba ya wanawake katika kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu na kuwapa nafasi kubwa ya kuendesha harakati zao, wamekua na nafasi muhimu katika uhudhuriaji na ushiriki katika ratiba mbalimbali zinazo beba ujumbe wa mapenzi na kuwatawalisha Ahlulbait (a.s) pamoja na kuhuisha utajo wao.
Miongoni mwa ratiba za wanawake –Kwa mujibu wa kamati ya maandalizi- ni kuendesha shughuli zao katika ukumbi wa Imamu Mussa Kadhim (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu zinazo beba mambo mengi, baada ya ufunguzi wa kikao chao ulifuata ujumbe wa ukaribisho kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu, halafu ikafuata hafla ya Qur’an ambayo walishiriki wasomi wa kike kutoka ndani na nje ya Iraq, kisha yakafanyika mashindano ya Qur’an tukufu, pia kulikua na wazungumzaji na wasomaji wa mashairi na qaswida za kuwasifu Ahlubait (a.s) kutoka kwa washairi raia wa Baharain na Iraq, miongoni mwa harakati zao pia walifanya maonyesho ya machapisho mbalimbali, ambapo walishiriki wanawake kutoka katika Ataba za Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya na Abbasiyya, walifanya na maonyesho ya picha pia.