Kama kawaida unapo ingia mwezi wa Shabani mtukufu ambao unabeba kumbukumbu ya kuzaliwa kwa miezi ya Alawiyya, wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kutoka India kila mwaka kwa kusaidiana na Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na ofisi ya Marjaa dini mkuu Ayatullah Shekh Bashiru Najafiy (d.dh), hufanya hafla.
Hafla imefanyika katika uwanja wa baina ya haram mbili tukufu chini ya anuani isemayo: (Kongamano ni subira na utekelezaji), imeendeshwa na kundi la waumini kutoka India watu wa mji wa Laknau (Maukibu ya watumishi wa bibi Zainabu –a.s-).
Hafla hiyo ilipata uhudhuriaji mkubwa kutoka kwa watu wa India na Pakistani waliokuja kufanya ziara wakiongozwa na muwakilishi wa Marjaa mkuu katika mji wa Banarus – India muheshimiwa Sayyid Shamim Hassan, aidha walishirikiana na ndugu zao wairaq na wengineo, pamoja na wawakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na mtoto wa Marjaa dini mkuu Ayatullah Shekh Bashiru Najafiy (d.dh) Hujjatu Islamu Ali Najafiy.
Mwisho wa hafla wasimamizi walitoa shukrani kwa kila aliye changia kufanikisha kwa hafla hiyo tukufu ambayo inachukuliwa kua ni miongoni mwa matunda ya kongamano la Amirulmu-uminina (a.s) la kitamaduni ambalo hufanywa kila mwaka na Atabatu Abbasiyya huko India.
Kumbuka kua kitengo cha (Maa baina haramaini sharifaini) kiliandaa eneo maalumu la kufanyika kwa hafla hii na kutengeneza jukwaa na kiliweka tayali watumishi wake kwa ajili ya kusimamia mwenendo wa hafla na kutoa msaada wowote utakao hitajika.