Siku ya pili mfululizo: Vikao vya kitafiti vinaendelea miongoni mwa matukio ya kongamano la Rabiu Shahada awamu ya kumi na tatu..

Maoni katika picha
Vikao vya kitafiti vinaendelea katika kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu linalo andaliwa na kusimamiwa na Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), asubuhi ya Juma Nne (5 Shabani 1438 h) sawa na (2 May 2017 m) katika ukumbi wa Sayyid Auswiyaau (a.s) ndani ya Atabatu Husseiniyya tukufu kilifanyika kikao cha tatu kilicho hudhuriwa na watu wengi wa sekula.

Kikao hicho kiliongozwa na Shekh Munjid Kaabi, kilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha zikafuata mada tatu za watafiti kuhusu shakhsiya na uongozi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), utafiti wa kwanza ulikua wa Shekh Mushtaaq Saidiy naye ni mwalimu katika hauza ya Najafu Ashrafu, utafiti wake ulikua na anuani isemayo: (Mafuhumu ya kujitolea katika mtazamo wa kimaumbile.. Abulfadhil Abbasi kama mfano), alielezea maana ya kujitolea kilugha na akatoa mifano mbalimbali, aya na riwaya zinazo zungumzia kujitolea, pia akaelezea kujitolea katika mfano wa akhlaq kwa kumtazama Abulfadhil Abbasi (a.s) na aliyo yafanya katika viwanja vya Twafu yaliyo mpelekea kua mfano mkuu katika somo la kujitolea.

Baada yake alifuatia mtafiti dokta Muhammad Na’anaa, ambaye ni mtafiti wa uhuru, haki za binadamu na demokrasia, utafiti wake ulihusu: (Utunzi wa sheria katika kupambana na makundi ya takfiri na ugaidi.. kulinganisha baina ya matukio ya Twafu na ugaidi) na akaelezea misingi ya kisheria katika mapambano ya imamu Hussein (a.s) na mitazamo ya makundi ya takfiri na ugaidi na vyanzo vyao vya kisheria pamoja na kutoa utatuzi wa kisheria katika kupambana na imani kali za ukufurishaji na ugaidi.

Kikao kilikamilishwa na mtafiti Ustadh Haidari Muhammad mwalimu wa lugha ya kiarabu, utafiti wake ulikua na anuani isemayo: (Uongozi wa mfano unapatikana kwa Abulfadhil Abbasi -a.s-), akaelezea mafuhumu ya uongozi wa mfano na misingi yake, akathibitisha kua sifa zote za kiongozi bora (wa mfano) zinapatikana kwa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kikao kilipokea michango mingi kutoka kwa washiriki na watafiti walisimama kujibu maswali na kusherehesha palipo hitajia kushereheshwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: