Mahafali ya Qur’an katika haram tukufu ya imamu Hussein (a.s) hitimisho la ratiba ya siku ya tatu ya kongamano la Rabiu Shahada awamu ya kumi na tatu..

Kisomo cha Qur’an
Mwisho wa ratiba ya siku ya tatu katika kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu, katika haram tukufu ya imamu Hussein jioni ya Juma Nne mwezi tano Shabani (1438 h) sawa na (2 May 2017 m) kimefanyika kisomo cha Qur’an pembezoni mwa kongamano.

Kisomo hicho kilifunguliwa na msomaji Falahu Zalif Usama Karbalai ambaye aliburudisha masikio kwa kisomo murua cha Qur’an tukufu, kisha akafuatia msomaji Said Saiid Muslim kutoka Misri hali kadhalika alivutia watu wengi kwa kisomo chake kizuri, halafu akasoma Usama Karbalai, akafuatia Haafidh Muhammad Ali Islami, kisha akasoma Mustafa Ghalibiy ambaye aliimba Qaswida za kidini, kisha akasoma Ahmad Abdulhayyi kutoka Misri.

Kamati ya maandalizi ya kongamano imepanga kufanya vikao viwili vya usomaji wa Qur’an tukufu, cha kwanza ni hiki cha leo na cha pili kitafanyika kesho –inshallah- katika uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na imai kua Qur’an tukufu ni muujiza wa kudumu alio kuja nao Mtume (s.a.w.w), bali ndio muujiza mkubwa zaidi alio pewa Mtume wetu mtukufu (s.a.w.w), nayo ni neema iliyo bakia kwetu na ni hoja ya nguvu na dalili ya wazi, pia ni nuru na taa isiyo zimika mwanga wake, aidha ni bahari ni isiyo julikana kilele chake, ni kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, ndani yake kuna uthibitisho na dalili za wazi kuhusu utume wake (s.a.w.w) na uthibitisho wa mitume wengine wote walio tangulia (a.s).

Mahafali ilihitimishwa kwa kutoa zawadi na vyeti vya ushiriki kwa wasomaji walio shiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: