Katika ukusanyaji wa habari ulio fanywa na mtandao wa Alkafeel wa kimataifa kwa wageni wa kongamano la Rabiu Shahada awamu ya kumi na tatu, wageni wanao muwakilisha mufti wa Iraq wameonyesha kuridhishwa na mazingira ya kongamano hili na wamesema kua; kongamano hili ni ujumbe wa amani kwa kila anaye lishuhudia duniani.
Shekh Sarmad Tamimiy muwakilishi wa mufti wa Iraq dokta Mahadi bun Ahmad Swamidaii amesisitiza kua: “Hakika kila mtu anafurahi anapoona waislamu wamekusanyika sehemu moja, kwa ajili ya kuuthibitishia ulimwengu kua wao ni waislamu, Mwenyezi Mungu mtukufu amewaita waislamu na sote tunapigana kuhakikisha jina la (Laa ilaaha illa Llah) linakua juu, kama ilivyo kwa imamu Hussein (a.s) mjukuu wa mtume wetu mtukufu, hili ndio alilokuja nalo na ndio alilo tenda na kwa ajili hiyo alijitolea muhanga, ili awakusanye waislamu katika (Laa ilaaha illa Llah), alikuja kunusuru dini ya babu yake, ambayo ni dini ya maingiliano, dini ya amani”.
Akaongeza kusema kua: “Kila anaeshuhudia kongamano hili tunamuambia hii ndio Iraq, Iraq ambayo imekusanya waislamu na wasio kua waislamu, na imekusanya waarabu na wasio kua waarabu sehemu moja, na tumeweza kuwaambia walimwengu kua sisi sio watu wa kutengana na mitafaruku, bali walio simama dhidi ya Ahlulbait (a.s) ndio watu wa kutengana na mitafaruku”.
Shekh Tamimiy alibainisha kua tunapasa kuwakumbuka Hashdi Sha’abi popote tutakapo kua, kwa utukufu wao leo hii tunakutana na kufanya makongamano kama haya, alisema: “Mwenyezi Mungu awanusuru Hashdi Sha’abi na awape ushindi mkubwa, Mwenyezi Mungu mtukufu amewateua ili wailinde ardhi hii na maeneo matukufu ya nchi yetu, tunamuomba Mwenyezi Mungu awape ushindi, na awafanye kua nguvu kubwa inayo tegemewa nchini kwetu na kwingineko, wamethibitisha kua wao ni baba, wao ni ndugu, mtoto na rafiki kipenzi kwa wote.